michibo
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 2,212
- 3,655
Naomba kupata ABCs za biashara ya bucha. Kuanzia vifaa vinavyohitajika gharama zake, vibali na upatikanaji wake.
Ikipendeza zaidi, basi na bei ya nyama machinjioni na makadirio ya faida kwa kilo. Na taarifa zote muhimu zinazohitajika.
Natanguliza shukrani.
=====
Mchango wa mdau
Ikipendeza zaidi, basi na bei ya nyama machinjioni na makadirio ya faida kwa kilo. Na taarifa zote muhimu zinazohitajika.
Natanguliza shukrani.
=====
Mchango wa mdau
Nadhani unaweza kuanza hivi:-
Mauzo
- Tafuta fremu nzuri iliyopo sehemu nzuri, labda 200,000/= kwa mwezi
- Nunua mizani labda 150,000/=
- Tafuta gogo 50,000/=
- Mapanga,shoka 30,000/=
- Friza 500,000/=
- TIN
- Leseni
Bei ya machinjioni huwa kuna tofauti kama ya 1000 na ile bei ya kuuza rejareja dukani,inategemea na mkoa n.k
- weka malengo ya kuleta kilo 50 kwa siku ili usilaze nyama
- Tafuta wateja wako wa kudumu,angalau 10 n.k wanaweza kuwa mama ntilie au wachoma mishikaki
- Kilo zinazobakia utawauzia wateja ambao sio wakudumu,wapita njia
Kama utapata faida ya 1000 kwa kila kilo, inamaana kwa kilo 50 kwa siku, utauza 50,000/=
50,000 x 30days = 1,500,000/=
Mapato na matumizi
Faida utakayobaki nayo ni Sh. 850,000/=
- Mapato 1,500,000/=
- Toa kodi 200,000/=, utabaki na 1,300,000
- Toa muuzaji 200,000/= baki 1,100,000
- Toa usafiri kwa mwezi 100,000, baki 1,000,000
- Toa umeme na maji 150,000; unabaki na 850,000
Ukiwa na magoli ya namna hiyo 20; utakuwa na mapato ya sh. 17,000,000/=
Mkuu,ingia vitani ukawe tajiri