Habari wana JF,
Nimekua kwenye mahusiano tangu mwaka 2014 na binti mmoja na nikabahatika kupata mtoto wa kiume 2015 mwishoni.
Alipata kazi mkoani mbali na ninapokaa. Tatizo kubwa kati yetu imekua ni mawasiliano kwa upande wa mwenzangu, japo najitahidi kumuunganisha na vifurushi, ni nadra sana kwa yeye kunitafuta au kunijulia hali.
Kuna siku niliugua mpaka kulazwa na mpaka natoka sijapata simu yake hata moja. Sasa nimekua na wasiwasi mkubwa hivi kweli ananopenda au lah maana hata yale mahaba tu yakuitwa baby, hny, mume, sikumbuki mara ya mwisho yalikua lini.
Ukimuuliza unanipenda jibu linatoka kwa shida na kisingizio kikubwa kwake ni kazi zimembana. Nikifananisha na mahusiano ya nyuma yote niliyopitia wanawake wana affection kubwa sana kwa wapenzi wao but hii imekua kinyume chake. Kitu ambacho sipendi; ni mwanangu kuwa na malezi ya pande moja kama mimi nilivyolelewa lakini hali halisi ndo kama ivyo.
Naomba ushauri wenu, nifanyeje kabla sijafunga nae ndoa.
Karibuni.