Naomba ushauri juu ya Internet ya Halotel na Vodacom

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Mimi ninatumia huduma ya internet kutoka Vodacom. Hapo awali huduma hii ilikuwa ya unlimited na nilikuwa natumia kwa mwezi mzima.

Leo hii nikinunua kifurushi cha shs.25,000 sana sana ninatumia kwa muda wa siku 16 au 18 kinyume na zamani nilikuwa natumia mwezi mzima na mtandao wao ni pole pole sana mpaka inaudhi.

Jana nimekutana na Jamaa akinunua kifurushi cha Halotel nikamweleza shida yangu, yeye akanishauri kuhama haraka kwa sababu zifuatazo:-

- Kwanza Halotel ina spidi sana
- Pili kwa hizo hela 25,000 ninazotumia kununua kifurushi cha Vodacom kwa Halotel naweza kutumia kwa miezi miwili.

Nawaombeni ushauri katika suala hili.
 
Mkuu Halotel ni habari ya mjini Mimi nilikuwa natumiaga Tigo kwenye net wanazingua sana wakati mwingine hawapo hewani BT Niko Halotel kwanza wana sped sana kwenye net alafu bando zao ni cheep
 
Asanteni sana kwa ushauri. Kuanzia kesho nahamia Halotel. Hii ndiyo faida ya Jamiiforums.
 
Back
Top Bottom