Naomba ushauri jinsi ya kuwa mjenga hoja na kiongozi mzuri

J wizzy

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
458
535
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24, natokea mkoa mmojawapo kati ya mikoa ya kusini.

Nina kipaji cha kuongea na kuzungumza sana, hata nikifika ugenini, sichukui muda mrefu sana ntafahamika mahala hapo kutokana na haiba yangu.

Pamoja na kuzaliwa mkoa x, ila sijawahi kwenda mkoani kwangu physically, ila kiroho nimeenda sana, nimekua nikifatilia maendeleo ya mkoa wangu kiujumla, nimekua nikiumia sana ninapoona maendeleo duni yaliyopo huku kukiwa na resources za kutosha kabisa kusaidia kupiga hatua.

Nina uwezo wa kuwa kiongozi mzuri tu na kuisaidia jamii yangu, na hiki ndo kilio changu.Kwa sasa nipo chuo mwaka wa pili, huku mkoani dodoma.

Hivyo naomba ushauri kwenu;

1: Nifanyaje ili niweze kuwa mjenga hoja mzuri zaidi???

2: Nifanyaje ili niwe kiongozi bora kwa jamii yangu???

3: Nitafikiaje ndoto hii ya kuwatumikia wananchi ili wafaidike na rasilimali zinazowazunguka?

N.B Ni mwanachama wa chama cha siasa, ila naamini zaidi katika kuwatumikia wananchi na kuwasaidia kutatua kero zao.Kwasababu, nikiwa kiongozi nitatatua kero za wananchi wote na si za wale wachama changu pekee.

Nawasilisha wakuu.
 
pamoja mkuu tujue kwanza tunasafishaje vyeti then tukifika uko mtaani ni kuviweka pembeni na kufocus mbele zaidi maana sio kwa hali hii ninayoiona:(:(
 
pamoja mkuu tujue kwanza tunasafishaje vyeti then tukifika uko mtaani ni kuviweka pembeni na kufocus mbele zaidi maana sio kwa hali hii ninayoiona:(:(
Sijakuelewa mkuu, ufafanuzi kidogo tafadhali
 
Back
Top Bottom