Naomba ushauri: Biashara nje ya nchi

Naomba ushauri: Biashara nje ya nchi

Mebuttefly

Senior Member
Joined
Feb 5, 2014
Posts
114
Reaction score
94
Nilikuwa naomba ushauri ,nahitaji kufanya biashara ya kusafirisha vitu vyakula nje ya nchi,kama vile karanga.dagaa,maharage,majani y chai,kahawa,ikiwezekanz hadi jamii ya matunda.Naomba kwa anaejua steps za kufata.
Asanteni
 
Mkuu nitakupa ushauri mdogo lakini unaweza kukusaidia

1. Jambo la kwanza kabisa kwa biashara hiyo, tafuta masoko yake ujirizishe nayo nje ya nchi.
2.Ukisha pata soko, sajili jina la biashara au kampuni ikiwa ni pamoja na TN n.k
3.Ukisha malizana na BRELA kusajili, nenda wizara ya viwanda na biashara kuomba lessen ya kusafirisha bizaa hiyo. Watakueleza ni mambo gan wanaitaji
4.Ukisha pata Leseni ya kusafirisha, na tayari una mziko unatakiwa kwenda nje, utatakiwa kwenda kwenye mamlaka husika hili kupata kibali cha kusafirishia kwa mfano kama unapeleka mazao kama dagaa, utatakiwa kuomba kibali cha kusafirisha kwa muda huo kwa mwanza kinatolewa pale nyegezi.
5.Kumbuka ikiwa unataka kusafirisha katika nchi za Africa mashariki, utatakiwa kujiandikisha kwenye ofic iitwayo chamber of commerce. hawa watakupa barua ya kuonyesha wewe ni mtanzania na bidhaa hiyo inatoka Tanzania. hii itakusaidia wewe unapo ingiza mzigo kwenye nch husika, hautaulipia ushuru badala yake utalipa vat, ya ongezeko la thaman tu ambayo ni 16% ya mali yako.

Yako mengi ila leo nakuchangia hayo mkuu ngoja wengine waje kukuongezea
 
Asante mkuu kwa ushauri wako kumbe ina process nyingi sanan.kwa mfano bara la ulaya.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom