Naomba ufafanuzi wa hii combination mpya ya CBM!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Heshima kwenu wadau makini!

Nilikitana na mtu mahali akanambia kulikua na utaratibu wa combination mpya CBM yaani Chemistry,Biology na Pure Mathematics!

Kama utaratibu huo upo nchini tayari umeanza lini? wajuzi mlioko sokoni tuambieni ukweli huo!

Je, atakayesoma combination hii anaweza kkusomea nini baadae akimaliza masomo?
 
Shule gani hiyo mkuu ina kombi hiyo? kuna madogo nataka kuwapeleka.
kama unataka wasomee udaktari sikushauri waende advance badala yake wapeleke college za serikali wakasomee medical officer deploma miaka 4 na certificate 2yearz akimaliza anapangiwa kwenye mazahanati au hospital
 
ni kweli mkuu kama kweli wana utaka udaktari hata ufamasia basi wawe na division. one ya pcb na si vingevyo najua vyuo vya private ada kubwa na. majority ya watanzania ni maskini vinginevyo wataenda kozi nyingine lakini si afya. hivyo advance ni kupoteza mda tuu. mimi yamenikuta.
 
Achane kudanganya wenzenu na combination za kijinga hizo hazipo,labda zitaanza mwaka huu! CBM?! Ni kwikwi
Good, ndicho kilichotakiwa kujibiwa mkuu! Sasa nilikua naona wadau wanazunguka shina la mti bila kupanda.
 
Hizo combi zilianzishwa na kufutwa mwaka juzi. Kulikuwa na combi mpya nyingi tu kama Physics,geograpgy na economics(PGE) Economics accountancy na maths(EAM) na zingine kibao. Ila zilifutwa na serikali so kama watazirudisha tena sijui
 
ni kweli mkuu kama kweli wana utaka udaktari hata ufamasia basi wawe na division. one ya pcb na si vingevyo najua vyuo vya private ada kubwa na. majority ya watanzania ni maskini vinginevyo wataenda kozi nyingine lakini si afya. hivyo advance ni kupoteza mda tuu. mimi yamenikuta.
Ni kweli haswaaa na kuchomoa div 1 PCB kwa shule zetu hizi za kuunga ni ishu. Mimi sikusoma PCB lakini Nina washkaji zangu wengi ambao nimesoma nao ndoto yao kubwa kuwa madaktari,bahati mbaya wakapata division 2. Wamejaribu vyuo vyote vya serikali wametemwa. Ikabidi tu wakasomee ualimu.
Kina wengine ikabidi wakasome tu diploma ya clinical officer (3years) baada ya kutokuwa na nia yoyote ya kusoma kozi zingine. Mimi nakushauri,kama ndoto yake kubwa ni kusomea udaktari basi mpeleke vyuo vya afya lakini kama ni kozi zingine,mpeleke Advance.
 
Back
Top Bottom