Naomba ufafanuzi kuhusu Udalali wa Mahakama ama Court Brokers

WEKKI

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
477
145
Habari za Majukumu. Huwa nasikia hii shughuli ya udalalai wa mahakama. Kuhusu usajili nimeshapata taarifa lakini kwa wanavyofanya kazi naomba wenye uzoefu nayo ama wanaoifanya ama wenye ABC zake tujuzane. Lengo ni kujua kuna mazingira gani ya kuifanya kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.

ASANTENI
 
sasa alokupa taarifa za usajili si ndo akupe na namna ya ufanyaji?? kwa nn akupe taarifa nusu nusu?
 
Habari za Majukumu. Huwa nasikia hii shughuli ya udalalai wa mahakama. Kuhusu usajili nimeshapata taarifa lakini kwa wanavyofanya kazi naomba wenye uzoefu nayo ama wanaoifanya ama wenye ABC zake tujuzane. Lengo ni kujua kuna mazingira gani ya kuifanya kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.

ASANTENI
Kuna kamtaji kakubwa kidogo uwe nako!uwe na yardi na mafunzo ya udalali wa mahakama ambayo hutolewa nadhani chuo cha Lushoto,Tanga.Pia uwe na tin na lesseni ila kwa maelezo zaidi nenda mahakama kuu masijala watakupa ufafanuzi zaidi.
 
Kibongobongo labda udalalie kesi za kuku, wenye mikesi mikubwa, watu hutokomea, kisha unaanza mambo bounty hunter.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Kwa kuwa unajua kuhusu usajili, twende kwenye namna ya kufanya kazi.

Kesi ya madai inapokwisha kunakuwa na mshindi na mshindwa, sasa kama kuna jambo mshindwa ameamriwa na mahakama kulitekeleza na asilitekeleze, mshindi wa kesi anaenda tena mahakamani kuomba kati ya mengine, nguvu itumike ili jambo hilo litekelezwe, kwa kuwa mahakama haifanyi kazi za nguvu hapo ndipo madalali wa mahakama sasa wanapoingia, unateuliwa ukatekeleze hiyo amri, mfano kubomoa nyumba au kuuza mali ya mshindwa nk. Gharama ya kufanya kazi yako zimeelekezwa kwenye sheria ya minada na mara nyingi ni makubaliano kati yako na mteja wako.

Kwa kuwa mshindwa aligoma kutekeleza amri usifikiri atakubali kirahisi amri hiyo kutekelezwa na mtu mwingine, hivyo lazima nguvu itumike, dalali uwe na mabaunsa wa kufanya kazi hiyo, upate ulinzi wa polisi nk

Sambamba na hilo la kufanya utekelezaji wa amri za mahakama, pia madalali hutumika kusambaza nyaraka za kesi (za mahakama) kwa pande za kesi. Nyaraka kama samansi, hati za madai nk. Si unajua mkiwa na kesi mara nyingi mnakuwa maadui!! Ili mdai asijepigwa risasi na mdaiwa anapopeleka samansi kwa mdaiwa basi hapa ndipo madalali wanatumika, sababu wao wanakuwa wapo kazini na hawahusiani chochote na ugomvi au madai ya mdai na mdaiwa. Gharama ya kupeleka wito ndani ya mji ni shilingi elfu 10 hivi.

Pia soma hapa https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=announcements/pdf&id=66 Tangazo limeeleza kila kitu
 
Msambaza Summons za Mahakama Kwa Wenye kesi..anajitegemea...na Dalali WA Mahakama anajitegemea...Kiufupi kuna Kazi za (COURT BROKER na PROSESS SERVER)
 
Back
Top Bottom