Naomba ufafanuzi kuhusu Kozi ya umeme VETA

Entreprenuare

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,616
1,714
Wakuu habari!

Kuna mdogo wangu, amemaliza form IV Arts.. naona yupo tu hapa nyumbani bila kazi yoyote.

Nimefikiria nimpeleke Veta chang'ombe akasomee umeme atleast mpaka level 3.

Sasa, naomba kufaham, hii kozi atachukua muda gani mbaka kumaliza level zote

Na vipi swala la demand ya hii kozi katika labor market , imekaaje?

Karibuni.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hongera kwa uamuzi mzuri. Kawaida kila level ni Mwaka mmoja, hivyo level I-III atachukua miaka 3.

NB: Kama hana cheti cha form four anaishia level II. Pia hata akiwa nacho kwenda level III ni hiari. Kuanzia tu hiyo level II unakuwa fundi unayetambulika na unaweza kujiajiri au kuajiriwa na TANESCO au Viwandani.
 
Kwanza ikifika mwezi wa nane nenda ukamchukulie fomu mapema. Kumaliza hizo level zote inaweza chukua miaka mitatu au miaka 5 kulingana na uwezo wake wa akiri.

VETA ili uvuke level inakupaswa upate 100% CBET yaan 99% unarudia mwaka. Lakini pia unaweza ukapa 100/% lakini uwiano wa masomo ya kawaida ukawa mdogo kuliko mwenzako unashindwa pata nafasi mwaka unaofuatia.

Unaenda field unakuja endelea level 2 mwaka wa tatu wake hii kutokana veta kuchukua idadi maalumu tu ya wanafunzi ila km nduguyo mwanamke atapata upendeleo miaka mitatu anaweza piga level zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Level atakuwa ameiva? Anaweza kumudu baadhi ya tenda

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Oh nilikuwa na maana akiishia level 2, anaweza kuwa vizur

Sent from my iPhone using JamiiForums
[/QUOTE Ndio kikubwa tu afaulu masomo yote ya kozi yake ili apewe VC2(cheti cha level II). UKIFELI HATA SOMO MOJA TU NDANI YA KOZI YAKO HUPATI HICHO CHETI CHA VC2
 
Iko hivi.
Level I&II Ni umeme wa majumbani yaani Domestic Electrical Installation. Kwa kila Level Ni mwaka mmoja. Ukifika mwaka wa pili yaani Level II Kuna mchujo ambapo utatahiniwa kwa kufanya mtihani wa VETA na endapo ukipata kitu kinaitwa VC1 basi Level III utaisikia tu kwa jirani labda Urisiti lakini ukipata VC2 basi sifa ya kujiunga na Level III inayodili na umeme wa viwandani unayo.

UNAIPATA VIPI VC1 na VC2 yaani VERIFIED CERTIFICATE 1&2 VETA kwa fani ya Umeme kuna masomo Kama 7 hivi, Sasa ukipata masomo yote kuanzia ufaulu wa Alama C inayoanzia 61 na kuendelea hiyo ndiyo VC2.

Ukifaulu somo la fani(umeme) kwa kupata hiyo Alama C na kuendelea afu mengine yote ukapata F basi hiyo huitwa VC1.

Hata ukipata masomo yote Alama A halafu fani ukafeli ukapata chini ya C basi hauna cheti yaani Ni sawa na mtu aliyehitimu Form 4 akapata Zero
 
Umeme una soko lakini asikalie fani moja, akihitimu ajifunze na fani nyingine pia zitamsaidia. Ni hayo tu
 
Iko hivi.
Level I&II Ni umeme wa majumbani yaani Domestic Electrical Installation. Kwa kila Level Ni mwaka mmoja. Ukifika mwaka wa pili yaani Level II Kuna mchujo ambapo utatahiniwa kwa kufanya mtihani wa VETA na endapo ukipata kitu kinaitwa VC1 basi Level III utaisikia tu kwa jirani labda Urisiti lakini ukipata VC2 basi sifa ya kujiunga na Level III inayodili na umeme wa viwandani unayo.

UNAIPATA VIPI VC1 na VC2 yaani VERIFIED CERTIFICATE 1&2 VETA kwa fani ya Umeme kuna masomo Kama 7 hivi, Sasa ukipata masomo yote kuanzia ufaulu wa Alama C inayoanzia 61 na kuendelea hiyo ndiyo VC2.

Ukifaulu somo la fani(umeme) kwa kupata hiyo Alama C na kuendelea afu mengine yote ukapata F basi hiyo huitwa VC1.

Hata ukipata masomo yote Alama A halafu fani ukafeli ukapata chini ya C basi hauna cheti yaani Ni sawa na mtu aliyehitimu Form 4 akapata Zero

Asante sana kwa maelezo mazuri sana

Kumbe veta hakuna mchezo mchezo.

Ila mimi naona bora asome mbaka level 3, ili awe vizuri kote kote, umeme wa majumbani na viwandani.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Oh nilikuwa na maana akiishia level 2, anaweza kuwa vizur

Sent from my iPhone using JamiiForums
Ni ujanja wako tu, kwa level II ni umeme wa majumbani tu lakini ukijichanganya kitaa na mafundi tofautitofauti utajua mengi Sana hata umeme wa viwanda bila kupiga level III japo class Ni mhimu
 
Iko hivi.
Level I&II Ni umeme wa majumbani yaani Domestic Electrical Installation. Kwa kila Level Ni mwaka mmoja. Ukifika mwaka wa pili yaani Level II Kuna mchujo ambapo utatahiniwa kwa kufanya mtihani wa VETA na endapo ukipata kitu kinaitwa VC1 basi Level III utaisikia tu kwa jirani labda Urisiti lakini ukipata VC2 basi sifa ya kujiunga na Level III inayodili na umeme wa viwandani unayo.

UNAIPATA VIPI VC1 na VC2 yaani VERIFIED CERTIFICATE 1&2 VETA kwa fani ya Umeme kuna masomo Kama 7 hivi, Sasa ukipata masomo yote kuanzia ufaulu wa Alama C inayoanzia 61 na kuendelea hiyo ndiyo VC2.

Ukifaulu somo la fani(umeme) kwa kupata hiyo Alama C na kuendelea afu mengine yote ukapata F basi hiyo huitwa VC1.

Hata ukipata masomo yote Alama A halafu fani ukafeli ukapata chini ya C basi hauna cheti yaani Ni sawa na mtu aliyehitimu Form 4 akapata Zero

Sijui sasa hivi lakini miaka ya tisini, mimi nilikataa kwenda form 5 mkoani , nikaenda Chang'ombe Electrical Installation, pale unapiga mwaka mmmoja kama ukiwa mzuri, wanachaguliwa wanafunzi wanne kwenda Moshi VETA, ambayo miaka hiyo ilikuwa bomba japo tuliowakuta Wakufunzi walisema miaka ya nyuma ilikuwa kama SWEDEN walimu wote walikuwa WASWIDISH.
Kati ya wanne wawili wanaenda Electronics na wawili wanaenda Industrial Electrical(umeme wa viwanda)
Nilipasua nikaenda Industrial Electrical japo nilipigwa zengwe sababu nilipasi vizuri kwenda Electronics, lakini baadae nilishukuru sana sababu miaka hiyo Electronics ningeenda kuwa Fundi TV na Radio.
Hiyo Industrial Electrical baada ya kumaliza kazi nilipata kabla hata sijapewa cheti na baadae ilinisaidia sana kama cheti cha kukubaliwa Chuo Kikuu kwa Bi Mkubwa na sikujutia hiyo kozi sababu nilipeta sana mwaka wa kwanza na wa pili wa Chuo.
 
Kwanza ikifika mwezi wa nane nenda ukamchukulie fomu mapema. Kumaliza hizo level zote inaweza chukua miaka mitatu au miaka 5 kulingana na uwezo wake wa akiri.

VETA ili uvuke level inakupaswa upate 100% CBET yaan 99% unarudia mwaka. Lakini pia unaweza ukapa 100/% lakini uwiano wa masomo ya kawaida ukawa mdogo kuliko mwenzako unashindwa pata nafasi mwaka unaofuatia.

Unaenda field unakuja endelea level 2 mwaka wa tatu wake hii kutokana veta kuchukua idadi maalumu tu ya wanafunzi ila km nduguyo mwanamke atapata upendeleo miaka mitatu anaweza piga level zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Myu awezi somea online
 
Back
Top Bottom