Naomba ufafanuzi kuhusu hii ya Kozi ya Petroleum Geology

Mr kilaja

Senior Member
Aug 21, 2016
110
64
Nilikua nauliza kuhusu kozi ya Petroleum Geology, inahusikaa na nini pia ajira zake,

Na je kozi hii inafungamana na Petroleum Engineering?
 
Nenda tu ukasome soko la ajira la mafuta na gesi litaimarika sana Siku zijazo
 
Petroleum geology (jiolojia ya petroli) ni jiolojia inayuhusika na utafutaji wa mafuta na gesi chini ya uso wa ardhi ya dunia. Watalaam wa jiolojia hii huwa wanafanya kazi ktk wa juu wa sekta sektafuta na gesi, na kazi yao kuyao huwa ni kutafta mafuta na gesi ktk mkondo huo. Watalaam hawa ajira zao zipo serikalini mfano TPDC pamoja na makampuni binafsi kama vile BG, STATOIL, SWALA, na makampuni mengine mengi yanayo tafta mafuta na gesi.

Petroleum Engineering (uhandisi wa Petroli) ni uhandisi unaohusika na uchimbaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi toka chini ya uso wa dunia. Wataalam wa uhandisi wa petroli nao pia wanafanya kazi ktk mkondo wa juu wa sekta ya mafuta na gesi. Wataalam hawa huwa wanapata data kutoka kwa wajiolojia wa petroli ili wajue sehemu ya kuchimba na kuzalisha mafuta na gesi.
 
Petroleum geology.. elimu ya miamba/madini na gasi/mafuta. Hawa wanatumika pia kwenye tafiti za uchimbaji wa visima/mabwawa..

Petroleum engineering... taaluma ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gasi..
Hawa ndo wana design namna ya kuchimba na production..
Hawa hawahusiki na maswala ya madini
 
Back
Top Bottom