Naomba tusaidiane malezi

Naomba tusaidiane malezi

toccara

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2014
Posts
540
Reaction score
203
Naomba ndugu zangu mnisaidie juu ya hili tatizo la huyu mtoto, Mwaka 2008 nilikuwa najitolea katika kituo kimoja cha watoto yatima baada ya kumaliza masomo yangu ya kidato cha sita, pale nilifanya kazi kwa moyo wangu wote kwa kuwa napenda sana watoto. Aliletwa mtoto mmoja wa kiume ambaye mama yake alifariki akiwa na week mbili toka kuzaliwa na baba yake hajulikani aliletwa na mama yake mkubwa kwa kuwa nae alikuwa hajiwezi kutokamna na kuumwa ugonjwa wa kisasa, basi nilikapenda sana hako katoto. Alivyofikisha miezi sita yule mama mkubwa alifariki na pale hakuwahi kujitokeza mtu mwingine kama ndugu hivyo mimi nikawa ndugu wa hiyari. Alivyofikisha mwaka alinizoea kwa kuniita mama, naenda chuo nikirudi namuwahi mtoto kituoni, nilianza tuu kumtania tania sister mkuu wa hapo kuwa namtaka yule mtoto. Ni story ndefu kidogo lakini Mungu alisaidia nilipata yule mtoto akiwa na miaka miwili ndiyo nilikabidhiwa rasmi ni mtoto wa kiume na nilimpenda sana na mpaka sasa ninavyoandika hivi ninampenda sana, sasa hivi ana umri wa miaka sita yupo darasa la pili, licha ya sasa nina watoto wangu wa kuzaa lakini huyu namchukulia ni mtoto wangu wa kwanza na mume wangu anampenda pia huyu mtoto.
Tatizo limekuja mwaka jana na nilipojifungua watoto wangu, huyu mtoto amekuwa na vituko vya kila aina na ana utundu uliopitiliza kiasi siwezi kusema najuta ila kiukweli naumia maana sina pa kumpeleka ni wangu. kituko cha kwanza alianza kuchana magodoro anatoa ile cover ya juu mpaka apate godoro lenyewe then anakata vipisi vidogovidogo kwa kutumia mkono vinakuwa vinji vinajaa ndoo kubwa, anapenda sana kuua wadudu na kuwaweka kwenye mfuko anawazika( hili nililifuatilia nikakuta ameshazika kama mafungu manne) anaweza kuwang'ata watoto wote au kuwapiga makwenzi., ukisahau kufunga chumba anaingia anapuliza perfume zote mpaka ziishe hili la perfume amelirudia jana usiku. kwa kweli anavituko vingi sana na sijapunguza upendo kwake kiukweli tunampenda sana.
Naombeni msaada weni nimfanye nini ili aache hivi vituko?
 
Kwanza Hongera pili pole tatu kwa umri wa miaka 6 bado anafundishika,muelekeze taratibu kwa upole na hekima kwa yale yasiokua mazuri.
Pia usimpende upendo wa kupitiliza sana utashindwa kumrekebisha.
 
kwa kweli upendo wangu umepitiliza, mimi nina watoto pacha wa kike tuu wawili na yeyey ni wakiume basi namuona kaka na kwa kuwa nimetoka nae mbali,sijui amejua kuwa nampenda sana, je kumchapa itasaidia?
 
Jaribu kuwa mkali kidogo atarekebishika..pia malezi ya dini yanamjenga sna mtoto ktk maadili mema..cjui imani yako
 
Pole mkuu! Inawezekana ni kipindi cha mpito tu,maana kuna umri fulani watoto huwa ni watundu sana.
Ila kama utaona anaendelea kama wewe ni mkristo,jaribu kumpeleka kwenye nyumba za ibada akaombewe maana unaweza kuta we unajua unajua mtoto kumbe si mtoto na yupo hapo kwako kwa kazi maalum ! Samahani kama ntakuwa nimekukwaza kwa lugha niliyotumia ila haya mambo yapo sana tu just believe me !
 
Maombi ni muhimu km ww ni mkristo ndyo silaha enyewe..uwe una mpeleka kwenye maombi atabadilika.sbb kuna tabia za kurith
 
imani yangu ni ya kikristu na nimemjenga vizuri
 
Maombi ni muhimu km ww ni mkristo ndyo silaha enyewe..uwe una mpeleka kwenye maombi atabadilika.sbb kuna tabia za kurith

ok, nadhani atakuwa hivyo, asante
 
kwa kweli upendo wangu umepitiliza, mimi nina watoto pacha wa kike tuu wawili na yeyey ni wakiume basi namuona kaka na kwa kuwa nimetoka nae mbali,sijui amejua kuwa nampenda sana, je kumchapa itasaidia?

sometimes viboko vinasaidia just mlee kama wengne unavyowalea ni wakwako huyo hata kama hukumbeba tumboni.usiwaze pa kumpeleka waza ufanyenin ili apunguze utundu, hata wakwako wanaweza kuwa hvyo,
kabla sijasahau hongera sana kwa kumuasili mtoto,may god bless u,ni wachache wanaweza,and plz usife moyo wala kufikiria mara mbili
 
Pole mkuu! Inawezekana ni kipindi cha mpito tu,maana kuna umri fulani watoto huwa ni watundu sana.
Ila kama utaona anaendelea kama wewe ni mkristo,jaribu kumpeleka kwenye nyumba za ibada akaombewe maana unaweza kuta we unajua unajua mtoto kumbe si mtoto na yupo hapo kwako kwa kazi maalum ! Samahani kama ntakuwa nimekukwaza kwa lugha niliyotumia ila haya mambo yapo sana tu just believe me !

hujanikwaza nimekuja hapa kuomba ushauri hivyo ninatakiwa kuuheshimu ushauri wako, hilo nami nilishaanza kulihisi cha ajabu niliambiwa shuleni kwao ni mpole sana, kazi iko nyumbani tuu
 
Hongera kwa moyo wa kipekee na Mungu akujaalie upate ufumbuzi wa namna ya kuwalea wanao wote.
 
sometimes viboko vinasaidia just mlee kama wengne unavyowalea ni wakwako huyo hata kama hukumbeba tumboni.usiwaze pa kumpeleka waza ufanyenin ili apunguze utundu, hata wakwako wanaweza kuwa hvyo,
kabla sijasahau hongera sana kwa kumuasili mtoto,may god bless u,ni wachache wanaweza,and plz usife moyo wala kufikiria mara mbili

asante sana kwa ushauri na pongezi zako
 
Nafikiri hiyo ni stage ambayo mtoto anatakiwa kupitia maana asipopita hapo mtasumbuana akiwa mkubwa hayo mambo atafanya mwisho atatulia tu wala usijali

ila uwe unamuonya kwa mambo ambayo anayafanya
 
ooh asante nilikuwa sijui
 
hongerah kwa unalotenda,kwa hiyo habari ya kuuwa wadudu na kupiga wenzie,sio bure tafuta hata nguvu za maombi kama alivyoshauri mjumbe mmoja!
 
Tatizo limekuja mwaka jana na nilipojifungua watoto wangu, huyu mtoto amekuwa na vituko vya kila aina na ana utundu uliopitiliza kiasi siwezi kusema najuta ila kiukweli naumia maana sina pa kumpeleka ni wangu. kituko cha kwanza alianza kuchana magodoro anatoa ile cover ya juu mpaka apate godoro lenyewe then anakata vipisi vidogovidogo kwa kutumia mkono vinakuwa vinji vinajaa ndoo kubwa, anapenda sana kuua wadudu na kuwaweka kwenye mfuko anawazika( hili nililifuatilia nikakuta ameshazika kama mafungu manne) anaweza kuwang'ata watoto wote au kuwapiga makwenzi., ukisahau kufunga chumba anaingia anapuliza perfume zote mpaka ziishe hili la perfume amelirudia jana usiku. kwa kweli anavituko vingi sana na sijapunguza upendo kwake kiukweli tunampenda sana.
Naombeni msaada weni nimfanye nini ili aache hivi vituko?

inawezekana kabisa ni njia ya kutafuta attention kutoka kwako hasa baada ya hao watoto wapya kuingia katika familia. Wataalamu wanashauri kuwaandaa watoto kabla ya wadogo zao hawajazaliwa na wategemee mabadiliko gani baada ya wadogo zao kuzaliwa na kuwa part ya familia. Mtoto wangu wa kwanza alibadilika ghafla baada ya mdogo wake kuzaliwa, alimpiga na kumfinya mdogo wake na alikuwa na miaka miwili na miezi kadhaa. hebu fikiria mtoto wa miaka sita atafanya nini atakapoona nafasi yake imechukuliwa tena na viwatu ambavyo hajawahi kuvisikia.

soma hiyo link inaweza kusaidia personally the information did help me.

Preparing your child for a new sibling: Overview | BabyCenter
 
naweza kusema kwa kweli huyu nimemuandaa toka nina mimba ya miezi mnne niliambia na doctor kufanya hivyo ikawa kila akitoka shule ananiuliza mtoto yuko wapi mama, namfanyia kama doctor alivyoniambia na mpaka tukawa tumejua wanaokuja ni wawili tukamweleza akafurahi sana kupata wadogo zake wawili ila alitaka aje wa kiume ili acheze nae mpira, nikamwambia wanakuja wadada wawili ila hakupenda waje wadada wawili alitaka na wakiume na mara nyingi anamdai wa kiume wa kucheza nae mpira nikamchukua mtoto wa kaka yangu wa kiume awe anacheza nae, kuna siku akamuuliza baba yeke (mume wangu) mbona huyu mdogo wangu wa kiume amekuja mkubwa mama hakuniita nimsikilize tumboni, hivyo anamadai yake. asante kwa ushauri
 
Back
Top Bottom