Naomba Shetta Usinirudishe Enzi za Mr Nice - Dudu Baya

geometry

JF-Expert Member
Oct 30, 2014
466
356
Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Dudu Baya amemtaka Shetta kuacha kutumia jina la ‘Mamba’ kwani hiyo ni ‘aka’ yake ambayo amekuwa akiitumia kwa miaka mingi.

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya alisema anaomba Shetta aache mara moja kutumia jina hilo ili yasije yakatokea kama ya Mr Nice.

“Shetta ni kama mdogo wangu sitaki ugomvi nae, asinirudishe enzi za Mr Nice,” alisema

“Mbona majina yapo mengi kwanini atumie jina langu (Mamba). Naomba afikishiwe huu ujumbe, nimemtafuta kwenye simu hapatikani,” alisema Dudu Baya.

Dudu Baya amedai ameona mara kadhaa msanii huyo anatumia jina lake bila kuongea nae.
 
Nimekumbuka hii kauli ya Julius Malema kwa Dr.Bonginkosi Emmanuel 'Blade' Nzimande ni baada ya Dr.Bongi kulalamika kwamba chama cha Malema (EFF) kimeiba rangi yao nyekundu kinayoitumia.

Nanukuu:

"Comrade Blade Nzimande is complaining that EFF stole the 'red color'

He doesn't have a copyright on the 'red color' and there's nothing we can steal from him because he has nothing but that skuurpot (pot scourer) face of his.

Why didn't he complain when Vodacom was red?"
 
Na yule aliyekuwa analia jina lake kutumiwa na mbwa wa Alikiba vimeishia wapi?
 
Kumbe ukitaka kuwa toa watu mafichoni dawa ni ndogo yani kumbe dudu yupo???????!
 
CCM nao wanambwa warudishe rangi ya Yanga kabla mafuriko hajahamia mtaa wa Lumumba.
 
dah,wabongo bana tuna visa!ka mr. blue nako kalilialia hapa kuhusu mondi kutumia jina la simba...yani mtu anaongea huku anatamani kulia kbs...wakati jina lenyewe muanzilishi ni afande sele.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom