Naomba Serikali waruhusu maandamano ya Dec 09,2025 na wayasimamie!!!

Naomba Serikali waruhusu maandamano ya Dec 09,2025 na wayasimamie!!!

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
6,929
Reaction score
6,030
Naiomba serikali yangu tukufu iyaruhusu maandamano ya Amani yanayotarajiwa kufanyika Dec 09,2025 kwa sababu wawaache watu watoe dukuduku lao kwa Amani.

Naamini kama Polisi wetu wanaweza kutoa ulinzi siku hiyo hakutakuwa na uvunjifu wa Amani katika maandamano hayo.

Kutokuyaruhusu maandamano hayo kufanyika kutaleta shida ya watu kubaka na dukuduku lao hivyo kupanga maandamano mengine siku nyingine kitu ambacho hakitakuwa kizuri kwa ustawi wa nchi yetu.

Ni kweli kabisa Mtukufu Rais alisema wamejipanga na wako tayari kupambana na maandamano hayo lakini mpaka lini nchi yetu itaendelea kuwa makini na maandamano wakati kuna kazi zingine ambazo askari wetu wanaweza kukaa na kuzifanya kwa manufaa ya Watanzania wote!

Maana kwa wiki hii tu kuna malalamiko mengi sana nchini kuhusu wanajeshi waliosambazwa nchi nzima kufanya mambo ambayo si mazuri kwa raia hasa huko Geita na vitongoji vyake kuna uonevu mkubwa sana unafanyika kwa watu na hii ni taswira si nzuri kwa Jeshi letu linalosifika kwa weledi.

Ili kuepusha haya yote ni vizuri sana Serikali yangu tukufu fikirie upya iwasikilize vijana iwaruhusu wafanye maandamano yao kwa Amani na Polisi au Jeshi wayalinde ili kusitokee uvunjifu wa Amani.
 

Attachments

  • IMG_3279.jpeg
    IMG_3279.jpeg
    184.4 KB · Views: 10
Back
Top Bottom