Naomba sana Rais Magufuli asiangalie chaneli ya Tanzania Safari

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,451
6,325
Ni kweli kabisa naomba sana mungu Rais asije siku akaangalia ile chanel ya Tanzania Safari ambayo imefunguliwa kwa mawazo yake na kuzinduliwa na waziri mkuu

Najua kabisa siku akiangalia atafukuza watu kazi yani nia uhakika wa asilimia 1000

Hii chanel tangu siku imezinduliwa mpaka leo naona cd yao ni hiyo hiyo moja, Makala zao ni hizo hizo tangu siku imezinduliwa

Hakuna kipya wala hakuna ubunifu wowote, its like mtu anaweka play then anaenda kulala

For sure ni aibu sana kwa inchi ya pili kwa utalii duniani kuwa na chanel ya utalii ambayo inaonesha uozo kama ule nasema tena ni aibu sana

Hivi ni kweli kabisa taasisi kubwa ya serikali wanashindwa kwenda mbugani huko au kokote kwenye utalii na kupiga kambi na kutengeneza documentary mzuri?

Mbona hata clouds tv wana kipindi chao cha kambi popote mbona kina mvuto sana nyie mnashindwa wapi? AIBU SANA
 
Inawezekana lilikuwa ndio wazo lakn wao kazi yao ni kuonesha cd zilezile utawakuta kila siku wanamuhoji askar Wa hifadhi yuleyule, hivi wanashindwa kwenda Serengeti au mikumi au hata ruaha kuchumua matukio ya wanyama

kabisa mbona wale jamaa wa clouds tv uwa wanafanya? sasa hii ni kwa vile ni serikali nilitegemea iwe Zaidi ya hapo
ni aibu kabisa kuna siku nimeona wanatangaza mbuga za Zambia na msumbiji kwa kuzuga ziko kwetu

mfano lao tangu asubuh tunaangalia oldzungwa tu na sauti ya shabani kisu, hakuna kingine
 
Nadhani tatizo ni bajeti, yaani hii kazi akipewa hata Millard Ayo naamini atatengeneza documentary nzuri zaidi.

swala la bajet hapana coz hii chanel ni wazo la Rais mwenyewe na pia hii ni chanel ya serikali na mbuga ni za serikali so hata gharama zitakuwa ni chache sana
 
watanzania hawajiongezi ndio maana rais anawatumbua kila leo. sio wachapa kazi wala ubunifu sana ubunifu wao ni lugha za mitaani kila kukicha neno jipya
 
Aisee Mimi mwenyewe nimeona ule ni uozo kwa kweli, yaani na aibu halafu mkurugenzi ni Dr Lyoba. Hivi kweli amekosa ubunifu kiasi hiki Dr mzima. Kumbe acha uncle awanyooshe nyumbu hawa. Sasa yeye kazi yake nini we unadhani kwa matangazo yale kuna mtu atavutia na hifadhi zetu kweli aje kutalii
 
kila jambo na wakati wake.
tayari ishatangazwa tender/invitation of interest ya watu binafsi/makampuni kuchukua slots za vipindi vyenye mlengo wa kutangaza utalii na kuitangaza nchi.
naamini with time mambo yataenda safi.
 
Mara mia ile Chanel wangepewa taasisi binafsi na sio tbc
😅😅😅😂, napendekeza apewe Millard Ayo. Kuna kipindi flani wakati ndio naanza kuiangalia sikujua kwamba wanarudia kipindi hicho day in day out, baada ya wiki kama 2 hivi nikakata tamaa baada ya kuona hawazalishi tena vipindi vipya,sasa sijui wanafikiri sisi watz hatuna akili au hao watalii tunaowavutia hawana akili ya kugundua kwamba hivi vipindi vinarudiwa au sijui wanatuchukuliaje...
 
swala la bajet hapana coz hii chanel ni wazo la Rais mwenyewe na pia hii ni chanel ya serikali na mbuga ni za serikali so hata gharama zitakuwa ni chache sana
Unakuja hakuna hela lkn?

Kwa sasa hela ziko huko kwny sector ya ujenzi&usafirishaji(vivuko,barabara,madaraja,barabara,ndege,kujenga meli,madarasa,airport).

Nyie mlioko kwny sector nyingine kama hizo za maigizo ya wanyama huko porini mpambane na hali yenu.
 
NAT GEO

ANMAUX.

hizi zinatosha.

Hiyo TANZANIA SAFARIS niliangalia Mara moja TU baada ya kuona wamemrekodi Rasta mmoja akiwa ametoboa masikio na pua huku kavaa heleni.
 
Back
Top Bottom