Naomba mwongozo: Rais anapopinga katiba nini kinafanyika?

baina

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
219
59
ibara ya 8 ya katiba hiko wazi juu ya nani ana mamlaka ya mwisho ya nchi hii, na rais aliapa kulinda hilo. je? kama sisi wananchi mpaka sasa hatutaki yeye aandae utaratibu wa kutunga katiba mpya bali sisi wananchi ndo tujipangie na yeye hataki kutusikiliza havunji katiba ya sasa ibara ya 8? au hajui? naomba kuwasilisha.:hug::hug::hug:
 
Nakupa mpaka j3 uje utueleze una ushaidi gani kusema rais anavunja katiba.. huo ndo mwongozo wangu mimi mh SPIKA!!!!!!!!!!!!!! La sivyo nitatumia vifungu kukusimamisha JF kwa muda usiopungua 2 yrs!!!!!!!!!! Mjadala umeahirishwa hadi utakapoleta ushahidi.. Tehe tehe heheheheh!!!
 
Kwa kweli muswada unaowasilishwa bungeni wiki hii hauna maana kwa sababu kuna vipengere ambavyo haviruhusiwi kujadiliwa kikiwemo cha "presidency". Hii inamaanisha mamlaka za rais na kinga dhidi ya rais pamoja na kutohoji matokeo ya urais zitaendelea kubaki kama zilivyo. Ni dhahiri viongozi wetu wanahofia kuandaa mchakato wa upatikanaji wa katiba huru kutokana na madudu waliyoyafanya wakiwa madarakani hivyo wanahofu kujiandalia kabuli lao wdnyewe. Nashauri kiwekwe kipengere kwenye katiba kitakachosomeka hivi "viongozi wote walioshika madaraka kabla ya kuanzishwa katiba hii (mpya) na wakati wa mchakato wa kuanzishwa kwa katiba mpya hawatashitakiwa kwa makosa yoyote waliyoyafanya wakiwa madarakani". Tukifanya hivi natumaini tutapata katiba nzuri.
 
Hivi kweli wabunge wamepata muda wa kuusoma huo muswada manake muda mreeefu walikuwa wakihangaika na kamati za bunge. Kwa kuwa wabunge wengi wa CCM watakuwa hawajausoma muswada basi nadhani CCM watakaa kama Party Caucus na kuupitisha muswada huu kwa idadi yao. Kwa CCM labda Ole Sendeka lakini wengine sijui!! Hapa watanzania tumeliwa mchana kweupee. Muswada mbaya wa mchakato wa kutunga/kurekebisha (ndivyo unavyosema) katiba utazaa katiba mbaya ambayo haitakidhi matarajio ya Watanzania.
 
Siku zote ukipewa nafasi ya kutengeneza kidonge (dawa) hakikisha kinakuwa kitamu kwani kuna siku utalazimika kukitumia. Endapo uongozi uliopo madarakani utachiwa nafasi kubwa katika maamuzi lazima utajipendelea kwa sababu katiba iliyopo inawanufaisha. Ni vizuri katika huu mchakato wa katiba itikadi za vyama zinatakiwa kuwekwe pembeni. Hii ni katiba ya watanzania wote. Kuna siku vyama vitakufa lakini nchi itadumu milele.
 
ibara ya 8 ya katiba hiko wazi juu ya nani ana mamlaka ya mwisho ya nchi hii, na rais aliapa kulinda hilo. je? kama sisi wananchi mpaka sasa hatutaki yeye aandae utaratibu wa kutunga katiba mpya bali sisi wananchi ndo tujipangie na yeye hataki kutusikiliza havunji katiba ya sasa ibara ya 8? au hajui? naomba kuwasilisha.:hug::hug::hug:

hebu nikumbushe hiyo ibara ya nane inasemaje.
Nilisahau kupasoma.
 
Kifungu cha 8 cha Katiba kipo hivi:

8
.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Kwa hivyo, ikiwa hii ni serikali ya watu, na serikali itawajibi kwa wananchi, ni wajibu wa serikali kusikiliza angalau wananchi wanataka nini na sio kuwaachia viongozi wa CCM (akiwemo raisi) kuwaamulia hatma yao.

ibara ya 8 ya katiba hiko wazi juu ya nani ana mamlaka ya mwisho ya nchi hii, na rais aliapa kulinda hilo. je? kama sisi wananchi mpaka sasa hatutaki yeye aandae utaratibu wa kutunga katiba mpya bali sisi wananchi ndo tujipangie na yeye hataki kutusikiliza havunji katiba ya sasa ibara ya 8? au hajui? naomba kuwasilisha.:hug::hug::hug:

Napenda kukukumbusha "Mwl.Nyerere alisema Rais ambaye hawezi kulinda KATIBA ya nchi yetu hatufai hata kidogo hatufai, Rais wa nchi yetu ni lazima alinde na kuitetea KATIBA"

Sasa kama JK imeonekana kuwa kashindwa kutete na kuilinda KATIBA kama alivyo apa, kwa kifungu hicho cha ibara ya 8, si huyo ni dictator live kabisa.
 
Unamfanya hivi:boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom::boom:
 
Sasa ndio wananchi muelewe wazi kabisa ni Chama cha namna gani kilichopo madarakani na umuhimu wa kukiondoa madarakani kwa kura zenu. CCM haiko pale Ikulu kwa manufaa ya mwanachi wa kawaida, iko pale kwa manufaa ya kikundi kidogo kilicho hodhi madaraka na sasa kinajaribu hata kuhodhi mustakabali wa nchi yetu.

Na ukijua nani yuko behind CCM ndugu yangu utalia machozi.

Ni hivi. Usitegemee CCM itakubali mabadiliko ya kweli ya Katiba ya nchi. Siku CCM inakubali mabadiliko ya katiba au Katiba mpya huo ndio mwisho wa CCM. Sasa kama wako madarakani unafikiri watakubali hayo yatokee ndugu yangu! TUMIA AKILI YAKO. Na JK sio mjinga kiasi hicho. Hawezi kukubali CCM ifie mikononi mwake. Yeye sio Gorbachev wa Tanzania.

Elewe pia kuwa CCM inawafuasu wengi sana katika watumishi, wafanya biashara, na kadhalika ambao kwao si rahisi kuunga mkono mchakato ambao utapelekea CCM ikatoka madarakani. They have a lot to lose. Na kwa ufahamisho, ndugu yangu, kwa Watanzania wa leo, wa sasa, kinachothaminiwa ni maslahi binafsi. Taifa baadaye. Ni jambo la kusikitisha, lakini ukweli ndio huo.

Mtu yeyote mwenye akili timamu, mwenye kuthamini demokrasia ya kweli hangethubutu kutunga wala kuwasilisha kama muswada hiyo sheria ya mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu kama ilivyotolewa. Lakini wako draftmen "watanzania" wametunga huo muswada na iko serikali ya "watanzania" wanaupeleke bungeni. NA KULE BUNGENI HUO MUSWADA UTAPITISHWA KUWA SHERIA kwa sababu wabunge wa CCM ndio wengi na wana maslahi kwa CCM kuendelea kutawala. Katiba ya sasa inawapendelea wao! Kwa kifupi KATIBA ISIYO YA WANANCHI ITAPITISHWA KWA MARA NYINGINE TENA. NA KWA SHERIA ILIVYO HUWEZI UKAPINGA MAHALI POPOTE. VYAMA VYOTE HAVIRUHUSIWI KUSHIRIKI KWA MAANA YA KUELIMISHA WANANCHI NA MAPENDEKEZO YATAPELEKWA KWA RAIS(M/Kiti wa CCM) PEKEE.

Mimi nasema kuwa hizi class struggles zitaendelea hata baada ya Katiba kuandikwa upya au kurekebishwa kwa matakwa ya CCM. Dunia imejaa mifano mingi sana ya mapambano ya wananchi dhidi ya serikali zao. Kinachoendelea mashariki ya kati ni mfano tosha. CCM ina sikio la kufa.

Katiba ya Wananchi itapatikana baadaye lakini sio hii na sio kwa mtindo huu. Kinachopelekwa bungeni ni sheria ya mchakato wa katiba ya CCM na JK.

MUNGU IBARIKI TANZANA.
 
Nguvu ya umma imiguuni pa kikwete na genge lake la mafisadi. Lakini nahakikisheni wana jf mwaka huu hautaisha salama kwa kikwete! Asipokimbilia uhamishoni basi ataungana na wenzake The Heg
 
Kwa kweli muswada unaowasilishwa bungeni wiki hii hauna maana kwa sababu kuna vipengere ambavyo haviruhusiwi kujadiliwa kikiwemo cha "presidency". Hii inamaanisha mamlaka za rais na kinga dhidi ya rais pamoja na kutohoji matokeo ya urais zitaendelea kubaki kama zilivyo. Ni dhahiri viongozi wetu wanahofia kuandaa mchakato wa upatikanaji wa katiba huru kutokana na madudu waliyoyafanya wakiwa madarakani hivyo wanahofu kujiandalia kabuli lao wdnyewe. Nashauri kiwekwe kipengere kwenye katiba kitakachosomeka hivi "viongozi wote walioshika madaraka kabla ya kuanzishwa katiba hii (mpya) na wakati wa mchakato wa kuanzishwa kwa katiba mpya hawatashitakiwa kwa makosa yoyote waliyoyafanya wakiwa madarakani". Tukifanya hivi natumaini tutapata katiba nzuri.
Ndugu, heshima kwako! Lakini GATUDANGANYIKI.. Hao wanaojiita viongozi wamependelewa vya kutosha, hakuna nafasi ya kuendelea kuwabeba. YEYOTE ATAKAYESHIRIKI KUWEKA KIFUNGU CHA HIVYO WANANCHI WATAMHESABU KUWA MSALITI. Kama ccm haitaki kuelewa kistaarabu, haitabembelezwa balil italazimishwa kuelewa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom