Naomba mumshauri kwa upole huyu kijana

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,821
48,976
Za asubuhi,

Ombi langu mshaurini huyu baba kijana nimetoa ombi na msimtukane mshaurini kwa upole mkimaliza nampa link ajisomee mwenyewe.

Huyu kaka kijijini huko alinipenda tokea nikiwa form one na yeye form 3 kiukweli mimi sikuwahi kujua kupenda na wala hiyo maana nilikuwa sina ila kijana inaonyesha alikuwa na real love kwangu barua nikiwa shule ananitumia na hela kwenye barua nakula hela zake lakini akitaka kunikiss namwambia ni dhambi na mama amenikataza.

Hili alikubali sababu anajua mama yangu ni mlokole na ni mkali nikimsemea ataenda washa moto pale kwao namnyima vyote ila pesa yake nachukua na tunapiga story sana tu ila hakuna kugusana ni dhambi na hapo mimi nimesoma girls japo fom two kuna mambo yalitokea lakini yeye siyo sababu nikachukia wanaume wote pamoja na yeye ila pesa yake sikuacha niliipenda.

Form four akaomba mchezo nikachomoa kwa kigezo kile kile cha dhambi na kwamba hanipendi mpaka ndoa kaka wa watu akakubali tukawa wapenzi wa mdomo tu nimeingia advance huku Dar shule ya dei nikapata kaboyfriend (h ahaha huyu sitasahahu tulikimbizwa na wanajeshi) story ndefu hapa basi jamaa yangu huyu wa kusubiri nikawa nampotezea ila nikiwa na shida ya hela namwambia ananipa kwa kigezo me ni mke wake kiukweli siwezi sema kama nilikuwa namchukia hapana.

Nikaingia chuo khee ndiyo majanga zaidi nikaamua kumla kibuti akajaribu kujiua kaka yake akamuokoa aisee nilisutwa na wachaga wale sitasahau na kuambiwa akifa ni juu yangu mmh any way sipendi kukumbuka.

Kwa sasa ana mke na watoto wawili na anaishi Mwanza juzi kanitafuta anakuja kuniambia kuwa anakosa amani hana furaha sababu anaamini mimi ndiyo mke wake na mbaya zaidi kamwambia mkewe kuwa ananipenda mimi sioni tabu yeye kunipenda ila tatizo lipo kwangu nimemueleza haya naona haelewi wakuu embu mfungueni macho.

1. Huyu kaka ni mtu mzuri mno mno yani hastahili mwanamke kama mimi na ningekuwa naye ningekuwa nimeokota embu kwenye mwarubaini lakini siwezi kuwa naye naona nitamtesa hata kama angekuwa hajaoa mmmh hapana nimejichekecha wee siku ya tano leo bado najiona sistahili hata chembe kuwa na kijana huyu he is so nice to have a person like me naomba wakuu muelewe na mumshauri.

2, Nimemwambia siwezi penda wanao kama mama yao anavyowapenda ila yeye anasema hakuna shida atawapeleka boarding naogopa kumpa za uso asijejaribu tena kujitoa duniani aache viumbe hawa wateseke.

3. Anasema yupo tayari kunipa chochote ni kweli anaweza sababu nakumbuka shamba la baba yake alilompa jina langu na lake lipo, mimi ni mlaghai jamani na sijui kama kabadilisha umiliki haikuwa ni hati ila makabidhiano naona kabisa njia ile ya kumchuna huyu kiumbe ila watoto watateseka na hii familia machozi yao hayataniacha salama mmmh sipo tayari.

4. Nitamtesa najua unanipenda sana ooh no sideserve.

Wakuu kama kuna nyongeza msaidieni huyu mutu asipoelewa sasa nifikiri namna nyingine kumpa tunda siwezi si kwa sababu naogopa mimi mkubwa kila aina najua siwezi ogopa ila tu naogopa kugandwa hahhaha najua mtabisha ila miaka kumi unafuatilia kitu kimoja any way wanaume mnajua zaidi.

Nb: Familia yake inanikubali sana sijui wanaona nini kwangu kwa kweli

Karibuni
 
za asubuhi , ombi langu mshaurini huyu baba kijana..nimetoa ombi na msimtukane mshaurini kwa upole mkimaliza nampa link ajisomee mwenyewe.

huyu kaka kijijini huko alinipenda tokea nikiwa form one na yeye form 3 kiukweli me sikuwahi kujua kupenda na wala hiyo maana nilikuwa sina. ila kijana inaonyesha alikuwa na real love kwangu barua nikiwa shule ananitumia na hela kwenye barua nakula hela zake lakini akitaka kunikiss namwambia ni dhambi na mama amenikataza...

hili alikubali sababu anajua mama yangu ni mlokole na ni mkali nikimsemea ataenda washa moto pale kwao... namnyima vyote ila pesa yake nachukua na tunapiga story sana tu ila hakuna kugusana ni dhambi.....na hapo me nimesoma girls japo fom two kuna mambo yalitokea lakini yeye siyo sababu nikachukia wanaume wote pamoja na yeye ila pesa yake sikuacha niliipenda...

form four akaomba mchezo nikachomoa kw kigezo kile kile cha dhambi na kwamba hanipendi mpaka ndoa kaka wa watu akakubali tukawa wapenzi wa mdomo tu .. nimeingia advance huku dar shule ya dei nikapata kaboyfriend (h ahaha huyu sitasahahu tulikimbizwa na wanajeshi) story ndefu hapa.. basi jamaa yangu huyu wa kusubiri nikawa nampotezea ila nikiwa na shida ya hela namwambia ananipa kwa kigezo me ni mke wake ... kiukweli siwezi sema kama nilikuwa namchukia hapana..

nikaingia chuo khee ndiyo majanga zaidi nikaamua kumla kibuti akajaribu kujiua kaka yake akamuokoa aisee nilisutwa na wachaga wale sitashahu na kuambiwa akifa ni juu yangu mmh any way sipendi kukumbuka ...
kwa sasa ana mke na watoto wawili na anaishi mwanza juzi kanitafuta anakuja kuniambia kuwa anakosa amani hana furaha sababu anaamini mimi ndiyo mke wake .. na mbaya zaidi kamwambia mkewe kuwa ananipenda me sioni tabu yeye kunipenda ila tatizo lipo kwangu nimemueleza haya naona haelewi wakuu embu mfungueni macho :;;

1. huyu kaka ni mtu mzuri mno mnoo yani hastahili mwanamke kama mimi na ningekuwa naye ningekuwa nimeokota embu kwenye mwarubaini.. lakini siwezi kuwa naye naona nitamtesa hata kama angekuwa hajaoa mmmh hapana....nimejichekecha weeee siku ya tano leo bado najiona sistahili hata chembe kuwa na kijana huyu...he is so so so so nice to have a person like me .. naomba wakuu muelewe na mumshauri ...

2, nimemwambia siwezi penda wanao kama mama yao anavyowapenda ila yeye anasema hakuna shida atawapeleka boarding naogopa kumpa za uso asijejaribu tena kujitoa duniani aache viumbe hawa wateseke...

3.. anasema yupo tayari kunipa chochote ni kweli anaweza sababu nakumbuka shamba la baba yake alilompa jina langu na lake lipo me ni mlaghai jamani na sijui kama kabadilisha umiliki ... haikuwa ni hati ila makabidhiano .. nona kabisa njia ile ya kumchuna huyu kiumbe ila watoto watateseka na hii familia machozi yao hayataniacha salama .. mmmh sopo tayari.

4. nitamtesa najua unanipenda sana ooh no sideserve....

wakuu kama kunanyiongeza msaidieni huyu mutu asipoelewa sasa nifikiri namna nyingine kumpa tunda siwezi si kwa sababu naogopa me mkubwa kila aina najua siwezi ogopa ila tu naogopa kugandwa hahhaha hah najua mtabisha .. ila miaka kumi unafuatilia kitu kimoja any way wanaume mnajua zaidi..

nb: familia yake inanikubali sana sijui wanaona nini kwangu kwa kweli
Nimewahi seat

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miss chagga

kwanza wewe kama kweli ulichokiandika unamaanisha endele kushikilia msimamo wako kamwe usimpe nafasi huyo kaka for the sake of his already made family

pili muulize ikiwa anaumizwa sana na upendo wake kwako wewe ambaye hujawahi hata kukaa naye,anafikiri yule ambaye ametoa maisha yake na kuwa tayari kuishi naye na kumzalia watoto ana hisia gani kumwelekea?

tatu muulize kuwa ikiwa alithubutu kutaka kumaliza uhai wake kwa ajili ya mtu ambaye hana hisia naye namna gani huyo mama ambaye kajitoa kwa ajili yake atajisikiaje kuachwa na mume wake mpendwa kwa ajili yako?
 
Maninner mbona kama niwewe mwenyewe???...Ila usifanye hivyo ni dhambi sana my dear...mwambie akuelewe pia mpe tunda siku moja kama kumwambia na mimi nakupenda ila siwezi kuwa na wewe kwani kitu gani shi ngapi umefanya hayo mara ngapi do ze needfull
 
miss chagga

kwanza wewe kama kweli ulichokiandika unamaanisha endele kushikilia msimamo wako kamwe usimpe nafasi huyo kaka for the sake of his already made family

pili muulize ikiwa anaumizwa sana na upendo wake kwako wewe ambaye hujawahi hata kukaa naye,anafikiri yule ambaye ametoa maisha yake na kuwa tayari kuishi naye na kumzalia watoto ana hisia gani kumwelekea?

tatu muulize kuwa ikiwa alithubutu kutaka kumaliza uhai wake kwa ajili ya mtu ambaye hana hisia naye namna gani huyo mama ambaye kajitoa kwa ajili yake atajisikiaje kuachwa na mume wake mpendwa kwa ajili yako?
yote haya atayaona sababu me nimeongea nimechoka... yani haoni uchungu kabisa jamani.. Mungu amsaidie jamani
 
Maninner mbona kama niwewe mwenyewe???...Ila usifanye hivyo ni dhambi sana my dear...mwambie akuelewe pia mpe tunda siku moja kama kumwambia na mimi nakupenda ila siwezi kuwa na wewe kwani kitu gani shi ngapi umefanya hayo mara ngapi do ze needfull
tunda anaweza niganda .. huyu kaka ni hatari linapokuja swala la miss chagga
 
Mkuu mpe papuchi kijana wa watu jamani... :D:D:D:D:D:D:D

Ok natania tu, ila kiukweli jamaa anakupenda kutoka moyoni kabisaaaa... Sijui ni mwanaume wa aina gani kwa karne ya sasa hivi anayeweza kumfuatilia msichana kwa miaka 10 bila kuambulia hata busu duuuh o_O. Kama ni mume wa mtu hapo pagumu kiukweli maana vitabu vitakatifu vinatutaka kila mtu kuheshimu ndoa! Sasa cha kufanya jaribu kukata mirija yote ya mawasiliano na yeye inaweza ikasaidia...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom