Naomba mtoe tip kwa wahudumu

Naomba mtoe tip kwa wahudumu

rodrigaz

Senior Member
Joined
Jan 4, 2015
Posts
185
Reaction score
200
Habari zenu ndugu zangu, natumaini muwazima! Leo ningependa kushare na nyie hiki nilichokiona. Naimani kina ukweli ndani yake.
Je unapokuwa kwenye mtoko, wewe hutoa tip kwa muhudumu kwa huduma nzuri aliyokupatia? Je ni kiasi gani wewe hutoa ukilinganisha na bili yako? Kwanini wengi hutoa tip kwa warembo tu kwakuwa tunawataka? Je ni sawa kumuacha kaka au dada mtafutaji bila tip? Unafanyaje unapokuwa na mpenzi wako na unataka kutoa tip kwa mdada au mkaka ikiwa wewe ni jinsia tofauti na muhudumu bila kuonekana kuwa unamtaka? Sidhani kama unaweza kumuacha ndugu yako sehemu yeyote anafanya kazi ya kuhudumu bila kumpa tip, wengine hawawezi kuacha kumpa tip mtu anayemfahamu, anatoka naye mkoa au kabila moja au alisoma naye? Vilevile kwanini huyu aliyepewa tip asielewe tu kuwa ile ni tip isiyotaka ya ziada, maana utakaporudi utachangamkiwa zaidi na hata kupewa namba mixer kujirengesha hasa kwa wadada!? Hii imekaaje wakuu?
 
Huu utamaduni wa tip una ulazima gani??? Sijawahi kuuelewa kabisa.

Huyu si muajiriwa? Si analipwa kwa huduma anayotoa???

Kwa Africa tusivyo wastarabu huu utaratibu utaleta madhara makubwa, wahudumu wakishazizoea sana hizo tip wakizikosa wanakuwa wezi, hivi karibuni nilikwepo Bonasera Mwanza muhudumu alizidisha Tsh 30,000 makusudi kabisa.

Ukifatilia wengi wanamichezo inayotegemea hizo tip, wakizikosa Inabidi wafanye ujanja ujanja.

Binafsi naona bora hiyo mnayoiita tip nimpe mama muuza mboga ambae anafukuzia faida ya 2000 kwenye mtaji wa 7000 ili apate mlo wa siku.
 
Akili za walevi bana hiyo tip ungepeleka kwa watoto yatima ingekuwa bora

Hapana unakosea, angalau hawa wameamua kuajiriwa wapate chochote, kuna mijitu mizima kibao inaomba mtaani kwa kujifanya vilema na bado hela tunawapa.
 
Kwani hawalipwi mshahara!?

Wanalipwa ndiyo, lakini mshahara wao haulingani na huduma au thamani yao. Ni ugumu wa maisha ndo unapelekea mtu kuwa barmaid. Sidhani kama angekuwa dada yako ungemruhusu kufanya kazi hii!?
 
Back
Top Bottom