Naomba msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 26, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimeangalia mwenendo wa sisi Watanzania kwa muda mrefu,mwenzenu si uelewi.Mtanzania mmoja akianzisha biashara fulani wengine tutaanzisha hiyo hiyo;Rais au kiongozi yeyote wa ngazi za juu serikalini akisema jambo ambalo hatimaye litatuumiza sisi wenyewe, tutanyanyuka kuandamana na kuliunga mkono;tukiletewa shule za kata ambazo malengo yake halisi ni ku dumaza elimu, tutawapeleka watoto wetu huko bila hata kulalamika,huku tukisifu na kusema shule za kata ni mkombozi wa maskini.Mlolongo wa tabia hizo ni mrefu mno.Lakini hasa kwa nini? Naomba msaada.
   
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ..Maono finyu tikerra. Watanzania wengi bado wana mtazamo finyu hata katika masuala mazito yanayohusu nchi yetu. Kikubwa nilichogundua ni kwamba wengi ni waoga wa kuhoji endapo kuna jambo wanalitilia shaka au kutoridhishwa nalo na pia kuna ambao wanafanya mambo kwa mazoea. Kwa hali ilivyo sasa Tz ni wazi kuwa serikali inawaburuza wanachi. Pamoja na politiki za watu wetu lakini kwa mwananchi wa kawaida anaweza kugundua wazi kabisa kuwa nchi imekosa muelekeo. Je, watz wako tayari kufanya mabadiliko kuepukana na jinamizi lililopo sasa? Kwa ufahamu wangu sijawahi kushuhudia serikali mbovu katika historia ya Tz. Hata Nyerere aliyechukua nchi wakati wa ujima hakufanya madudu kiasi hicho.

  Nawahimiza watz kwa kweli kuna haja ya kufanya mabadiliko CCM imetupotezea muda sana jamani..Please Tanzanians "wake up"!!!!
   
Loading...