Kuna wanaume wengine wapo kwenye mahusiano na mwanamke .. hali mbaya.. akianza kupata mafanikio tu anamuacha mwanamke ambaye aliyekuwa anamvumilia anatafuta wanawake wengine.. MAHUSIANO ni ovyo tu kiujumla usiwalaumu WANAWAKE.. mzee na mimi ndugu yako hali mbaya nilitaka hata nisikoment huu uzi sema hii koment imenishawishi.. sina kitu mbaba..
Binafsi nimecomment kulingana na situation ya mleta mada maana ishu ya ndoa ukianza kuandika hapatatosha lakini niliona nicomment kulingana na huyo mwanamke alichomfanyia mshkaji na kuacha Hadi mtoto hii sio sawa kabisa aisee.
Wengi tunapitia hizi Hali na ukikaa na wanaume wengi utajua Wana matatizo makubwa Ila huwa tumeumbwa kunyamaza na wanawake wanatumia hii fursa kufanya unyama wao.
Wapo wanaume wanakosea wake zao hii ipo tu, wako pia wenye sababu zao mfano mtu Kama huyu mleta mada hata mwanamke akimrudia just in case kwamba walee mtoto huyo mwanamke akilalamika bado mwanaume atalaumiwa tu Ila huwa tunanyamaza tu.
Ukweli ni kwamba, mtoto wa kiume hana pa kusema matatizo yake ndio maana huwa tuna maamuzi yetu mtu unamlisha , unasomesha yeye na ndugu zake na watoto, unahangaika kujenga nyumba , unamnunulia na gari lakini anakuwa hawezi kushukuru hata kidogo.
Mwisho wa siku unaenda unakokuwa appreciated, Kuna mademu ukimpa laki mbili anakutunza na anakuheshimu mno, ukimlipia vyumba viwili na sebule anamuona Kama wewe ni mwokozi wake Ila unakaa na mshenzi hajui hata kusema mume wangu Asante kwa kututunza japo ni wajibu Ila just show appreciation.
Sasa ukose hela ananuna badala ya kuwa comfort, hata TV ukishika remote anaanza kulalamika tu tunaangalia tamthilia, hivi mwanaume gani atakaa na hiyo umbwa?
Ukifanikiwa kuachana na wanamke wa hivyo kabla hujamuua shukuru Mungu hata kama unalala njaa.