Naomba msaada wa tatizo langu la hedhi

Naomba msaada wa tatizo langu la hedhi

Habari za asbuh wakuu!

Nahitaji msaada wa hili suala, tatizo nivkwamba nikiwa naingia zangu mwezini period inakuwa ni nzito sana yaani inakuwa kama imeganda ganda halafu ni nyeusi mno.

KILA nikienda hospitali napewa dawa hali inakuwa ni ile ile tu kama kuna hospital nimeenda juzi ndio kabisa nikapewa dawa za uzazi wa mpango.

Angalizo mimba sijawai kutoa.

Mwenye kujua dawa anisaidie tafadhari
Pole ,miziz ya mpera na miziz ya mbaazi kata vpande vdogovdogo chemsha kunywa 1×2 sku 3 tu lete majbu

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Habari za asbuh wakuu!

Nahitaji msaada wa hili suala, tatizo nivkwamba nikiwa naingia zangu mwezini period inakuwa ni nzito sana yaani inakuwa kama imeganda ganda halafu ni nyeusi mno.

KILA nikienda hospitali napewa dawa hali inakuwa ni ile ile tu kama kuna hospital nimeenda juzi ndio kabisa nikapewa dawa za uzazi wa mpango.

Angalizo mimba sijawai kutoa.

Mwenye kujua dawa anisaidie tafadhari
Habari,

Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia ili kuweza kusema kuwa kuna shida kwa kiasi/namba ya pads kwa siku, rangi, umri wa kuvunja ungo na idadi ya siku za damu kutoka. Hivyo, ni pale ambapo haya yote hapo juu yakijumuishwa kutakuwa na mwanga zaidi.

Kwa ujumla:
Zao la kiasi cha damu kinachotoka, hutegemea na kiasi cha unene wa ukuta uliojengwa kama maandalizi ya mji wa mimba na uwezo wa mishipa ya damu kufunga baada ya ukuta ule kutoka/mfumo wa kuganda wa damu mwilini. Hii pia hutegemeana kwa mtu mmoja kwenda mwingine.

Kwa mabinti ambao wametoka kuvunja ungo kupata damu ambayo imepoteza rangi ya asili inaweza kuchukuliwa kama hali ya kawaida kama hakuna dalili nyingine zinazoandamana na hilo, kwani viungo vyote: matezi na mji wa mimba huwa vinaendelea kujifunza kwa tukio husika.

Kuharibika kwa damu ya hedhi kwaweza kusababishwa na:

1: Kiasi kidogo cha damu ambayo ni zao la kiasi cha ukuta kilichojegwa na hivyo huwa na flow/ utokaji wa taratibu pamoja na yote yaliyotajwa hapo juu.

2: Msukumo mdogo wa mji wa mimba kutoa zao kile kilichoko ndani, kutokana na damu au zao la kubomoka kwa miji wa mimba kuwa kidogo.

3: Uvaaji wa pedi au vifaa vinavyotumika kujisitili uliobana na kuzuia flow/utokaji huru wa damu husika.

4: mimba iliyoharibika bila ufahamu wa muhusika. Bado kuna mimba ambazo uharibika bila akina mama kutambua kuwa walikuwa wajawazito. Hayo hutokea pale wanapopitisha aiku zao tarajiwa na wakiwa wamejihusisha na kujamiiana.

5: Matatizo ya kimaumbile ya mji wa mimba.

6: Matatizo ya mfumo wa homoni.

Kama hakuna dalili nyingine, basi ni vyema kuwa kwenye uangalizi wa kumwona daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama.

Kwa umri ulionao kama hakuna shida nyingine ni vyema kuendelea kuwa kwenye kufuatilia tu bila kufanya mengineyo.

Ni vyema unapopewa dawa kupata maelezo ya dawa ni kwaajili ya tatizo lipi na ni nini matarajio.
 
Ahsante mkuu
 
Back
Top Bottom