Salamu.
Natumia Laptop internet ya WiFi, tatizo ni kwamba nikifungua browser yeyote najikuta inafunguka na hiyo website ya kiarabu na maelekezo yote yanakuwa kwa lugha ya Kiarabu. Nilitafuta suluhu kwenye Google nikakuta maelekezo ya kuiondoa kwenye browser ya Chrome kwa kuifuta kwenye option ya "manage search engine", hata hivyo nilivyojaribu kuifuta nikapata error message kwamba "This setting is enforced by your administrator". Mimi ndiyo mwenye LapTop na ndiyo Administrator sasa nimeshindwa kuelewa kwa nini nanyimwa haki ya kufuta.
Naamini nitakuwa nimejieleza vema.
Natanguliza shukran Chief Mkwawa