pmuta
JF-Expert Member
- May 9, 2016
- 787
- 600
Nilifungua kesi ya jinai juu ya raia mmoja wa kigeni toka mwaka jana. Kesi hii ilichelewa sana kufika mahakamani hii ni kutokana na raia huyu kuwa alitengeneza mazingira ya rushwa kwa OCS na OCD ambapo waligoma kupeka faili mahakamani.
Nilimuandikia RPC na kwenda kumuona direct lakini bado haikusaidia maana bado raia huyu alitengeneza mazingira mpaka ngazi ya RPC. Ikabidi nimuandikie barua IGP na kumcopy Mkurugenzi wa makosa ya jinai na Waziri wa mambo ya ndani ndipo faili lilishinikizwa kupeleka mahakamani ambapo imepangwa kusikilizwa tarehe 24/02/2017 toka ifike mahakamani.
Binafsi skuwahi kupewa taarifa na huyo Mzungu ameattend mahakamani mara 3 ambapo alipewa dhamana. Mimi nimepewa tu taarifa nifike tarehe husika. Kesi hii iko mahakama ya Wilaya ila kwa mazingira haya tayari nimemuandikia Mh Jaji mfawidhi ili ikimpendeza aweze kutoa maelekezo kesi hii ihamishwe na kusikilizwa sehemu nyingine.
Kesi hii ina mashaidi wawili ila nilichokigundua inaonekana mashaidi hawa tayari wameshapewa pesa ili wasifike mahakamani.
Sasa naomba kujua, je ikiwa hawatafika mahakamani maelezo yao walitoyatoa ambayo yapo kwenye faili yataweza kujitosheleza kuwa ushaidi juu ya shauri hili?
Msaada wenu tafadhali. Kesi hii ilifunguliwa mwaka jana toka January na imefika mahakamani baada ya miezi 10.