Naomba msaada wa kisheria kuhusu matunzo ya watoto

giftally

New Member
Apr 19, 2020
3
1
Salama ndugu zangu,

Naomba ushauri wa kisheria Kwa hili swala,dada yangu ni mama wa watoto 2,wakike na kiume,miaka 6 na 3,alikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu kidogo kama miaka 10+ lakini hakukua na ndoa.

Kwa kifupi ni yale mahusiano ya on and off, mwishoe watoto wakahusika Mwaka Jana mwanzoni, mwanaume akahamia nje ya Tanzania kikazi (serikalini) matunzo ya watoto yakaanza kusuasua.

Kifupi matumizi ya watoto mapaka kupigizana kelele, kifikia mwezi wa 10 mambo yamezidi kuwa mabaya,dada alikuwa mfanyakazi pia,lakini kutokana na kulea watoto na wakati mwingine kukosa wa kumwangalia watoto wawili,akasimama kazi. Msaada unaoomba ni kujua:

1. Kama mtu yupo nje ya nchi kumshitaki inakuwaje? Unatumia njia gani?

2. Tunaomba kujua sehemu sahihi pia ya kushtaki ni ustawi wa jamii,dawati la jinsia, LHRC,au sehemu gani haswa?

Tunatanguliza shukrani.
 
Nenda ustawi wa Jamii Utapewa Ushauri pakuanzia. Halafu mshauri Dada yako awe makini utazaaje na mtu bila kuolewa?
 
Sasa hutaki kuzaa kwanini usitumie Kinga Mana hapa umelaumu mwanamke tu wakati zinaa ni za wote hutaki kuzaa na mtu andikishianeni kabisa na muwe makini.

Mana mtu una mke husemi mnajiachia tu baadae ukibanwa mnalaumiana, acheni kutesa wanenu bwana kwa zinaa G'taxi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini msiende kazini kwake kwa kuanzia. Si unasema yuko serekalini? Nenda kazini kwake omba kuonana na mkuu wake wa idara muelezee kinagaubaga kisha yeye atakuwa kwenye nafasi nzuri sana kumpata jamaa kwa mawasiliano zaidi.

Nimeshauri kwa kutegemea kuwa nimeamini upande wako wa habari, maana unaweza kumsikia jamaa akakupa habari tofauti kabisa na hii. Kuna kipindi kina mama huwa mnalipuka sana.

Mara nyingi ukishazaa na mtu unahisi umeshika mpini na jamaa kashika makali na huwa hamjali tena kama jamaa ana familia au vyovyote mnakuwa na mashindano yasiyo na maana na kauli za hovyo sana sasa mkikuta jamaa nae dakika tatu 3 anawaachia manyoya tu.

Unapozaa na mtu na akaamua kulea mtoto wake, tulia na usijiinue. Usianze kujilinganisha na mke wa ndoa! Ukianza ku compare wewe na mke wa ndani ya ndoa au kwa kuwa jamaa unajua mshahara wake ni milioni 4 unalazimisha sasa lazima milioni 2 zitunze mtoto wako!
 
So unataka kusema wewe kua huyo bwana ndo mwenye makosa na mwanamke hana kosa? Jinga kabisa wewe...mwanamke ana hiari ya kukubali au kukataa na hatalazimishwa,amezaa kwa matakwa yake kwa kigezo cha udhaifu wa mwili wa mwaanaume,acheni upumbavu
Sasa hutaki kuzaa kwanini usitumie Kinga Mana hapa umelaumu mwanamke tu wakati zinaa ni za wote hutaki kuzaa na mtu andikishianeni kabisa na muwe makini. Mana mtu una mke husemi mnajiachia tu baadae ukibanwa mnalaumiana, acheni kutesa wanenu bwana kwa zinaa

Sent using Jamii Forums mobile app

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
G'taxi,
Kaka hii hata haihusiani na kujibebesha mimba, ilikuwa relationship nzuri Tu ambayo labda haiishii vizuri, sidhani kama mtu anaweza kutegeshewa mimba za watoto wawili, ndoa pia zinavunjika tu mbona, hamna mtu kalazimishiwa watoto ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom