Naomba msaada wa kisheria katika suala hili la Mzazi wangu kudhulumiwa stahiki zake

omboklo

Member
Mar 9, 2020
45
125
Habari za majukumu wakuu, natumai tunaendelea kuchukua tahadhari zote ili kujikinga na janga hili la corona.

Ningependa kuelewa sheria inaweza kufanyaje kazi katika jambo hili lililoweza kumkabili mzazi wangu.

Ilikua mwaka 2018 mwishoni baba yangu alipata wazo kutoka kwa binamu yangu kuwa wafungue Chuo cha Udereva na kwa namna alivyoelezewa ilimpa hamasa sana ya kuinvest pesa zake akiamini kua ni ndani ya miezi miwili pesa zake alizotoa zitakua zimerudi na wataanza kutengeneza faida, katika kipindi hiki chote hakuwahi kutushirikisha watoto wake tumekua tukipata taarifa tu kupitia kwa mama yetu.

Taratibu za kusajili zilianza na kipindi chote yeye alikua akituma pesa kwa binamu yangu ili aanze michakato, alifanikiwa kukamilisha kwa koasi kikubwa na mwaka 2019 mwezi wa pili chuo kilianza kutoa masomo mambo yalikuwa vizuri na mawasiliano yalikua mazuri ila ndani ya mwezi mmoja hali ilibadilika baada ya pesa kutokuoneka nikimaanisha kua kazi inafanyika ila pesa zilikua zikiingia kwenye akaunti ya huyo binamu yangu.

Baba aliweza kuomba kujua hesabu na ikiwezekana pesa iwekwe kwenye akaunti ya kampuni lakini jambo hilo halikuwezekana ulitokea mvutano mkubwa kiasi kwamba ndugu waliingia kusuluhisha lakini halikuwezekana jambo lolote na hadi leo ni mwaka sasa umepita mzee hajawahi pata return yoyote kutoka kwa hiyo biashara na hajui namna inavyoendelea.

NB: katika usajil binamu alitumia jina lake kwahiyo nyaraka zote zinamuonesha yeye ndio mmiliki ingawaje pesa zilitoka kwa baba.

Ninapenda kujua je ni namna gani sheria inaweza kutusaidia ili tuweze angalau kurudisha pesa hizo zilizopotea (ushaidi uliopo ni slip za benki ambazo alikua akimuwekea pesa benki kwa ajili ya kuanzisha hiyo kazi).

Natanguliza shukrani.
 
Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,764
2,000

Poleni sana,

Unahitaji ushahidi zaidi, kama baba aliweka pesa kwenye akaunti binafsi je tunawezaje kujua kuwa hakuwa anamwekea pesa kwa ajili ya matumizi mengine/binafsi?

Ushahidi zaidi unahitajika kufafanua nafasi ya mzee katika kampuni.

Nakushauri tafuta mwanasheria akuchimbie zaidi, akuoneshe nafasi ya kesi yenu kabla ya kuamua kushtaki.

Kimsingi maelezo yako yanaongeza maswali zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru pia kwa muongozo huoo

Kwa hali ilivokua ushahidi pekee wa dhahiri uliopo zimebaki kuwa msg ambazo wamekua wakitumiana na pia kuna jumbe zingine amekua akitutumia hata sisi watoto kuconfess kua atalipa hizo pesa.

Je kwa ushahidi huo unaweza kutosha ama tuzidi chimbua zaidi.
 
Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,764
2,000
Nashukuru pia kwa muongozo huoo

Kwa hali ilivokua ushahidi pekee wa dhahiri uliopo zimebaki kuwa msg ambazo wamekua wakitumiana na pia kuna jumbe zingine amekua akitutumia hata sisi watoto kuconfess kua atalipa hizo pesa.

Je kwa ushahidi huo unaweza kutosha ama tuzidi chimbua zaidi.
Ujumbe mfupi pia unaweza kutumika kama ushahidi, lakini kumbuka pesa zote ziliwekwa kwenye akaunti binafsi.

Kama nimekuelewa vizuri tunataka kudai mchango wa baba katika shule ya udereva, ambayo awali baba alichangia akidhani taarifa zote zinatunzwa katika umoja wao wa yeye na mdaiwa, lakino la. Ambapo shule ina usajili, pesa ziliingia kwenye akaunti binafsi n.k

Mbali na kukiri kuwa atazilipa pesa, kuna maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kupata msimamo wa swala zima. Mfano kiasi (pesa+nguvu kazi)gani kila mtu alichanga n.k. je katika msgs anakiri atalipa kiasi gani/kipi-je anachotaja na alicholipwa vinaendana n.k

Hapa ninazidi kukuelewa, inapaswa tuzidi kukusanya ushahidi ili ataje kiasi kamili ambacho atalipa maana katika ushahidi wa awali hakuwahi taja kiasi anachodaiwa zaid ya kukiri kua anadaiwa.

Nakumbuka yeye kikubwa alichofanya ilikua ni kuhakikisha taratibu za usajili zote zinakamilika nikimaanisha kua kias cha pesa kilichotumika hadi kukamilisha hiyo shule kilitoka kwa baba.

Nashukuru nimepata mwanga zaid
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom