Naomba msaada wa kisheria katika hili

skata jr

Member
Jan 15, 2017
18
6
Kuna binti nilizaa nae mwaka 2012 lakini nikiwa bado nasoma chuo mwaka wa kwanza BA, binti kwasababu alikuwa bado anaishi na walezi wake hakutaka kunitaja mapema, kwani alikuwa anajua hali yangu nakunionea huruma kama wangeamua wamfukuzie kwangu basi ndoto zangu pia zingeweza kuishia njiani.

Nikiwa na karibia kuingia mwaka 2 niliamua kwenda mwenyewe kwa walezi wake kupitia wazazi wangu, wazazi wangu walipangiwa laki tatu 300000/= hiyo hela ilihusishwa na matibabu ya mama wa mtoto akiwa mjamzito, kwa wakati huo hela hatukuwa nayo kwa hiyo likabaki deni, nimemaliza chuo nimejitahid nmetafuta hela ile nimepeleka wanadai eti imeongezeka kwa sababu nieichelewesha, na mtoto kwa sasa ni umri wakwenda shule, niitaka nimepeleke shule nifanyaje?
 
Msomeshe mtoto shule na mama yake fanya utaratibu wa mahari umpose uishi nae huyo ndio mkeo halali. Alikujali na kukuthamini sana......
 
Lipa kwanza deni na kama kuna mlikubaliana siku ya malipo, (as a reasonable man) ulitakiwa kujua consequencies of the delayal. Ila kama hamkukubaliana deadline na wao walielewa hali yako, basi wanakosea kukupiga fain. Na huyo mtoto umpeleke shule.
 
Hapo kuna suala gani la kisheria la kutuita Wanasheria? Hilo ni suala la kijamii. Unapaswa kulipa pesa unayoambiwa. Amasivyo, unapaswa kumchumbia na kumuoa huyo dada ili hiyo hela ipungue kwakuwa atasaidia kueleza kwa ndugu zake. Huna namna nyingine zaidi ya kulipa unachopaswa kulipa.
 
Ahsante nimekuelewa mkuu... Hakukuwa na makubaliano yeyote kuhusu muda
 
Hapo kuna suala gani la kisheria la kutuita Wanasheria? Hilo ni suala la kijamii. Unapaswa kulipa pesa unayoambiwa. Amasivyo, unapaswa kumchumbia na kumuoa huyo dada ili hiyo hela ipungue kwakuwa atasaidia kueleza kwa ndugu zake. Huna namna nyingine zaidi ya kulipa unachopaswa kulipa.
Suala ni kwamba baba ake mdogo ndo mtata kifup amekuwa kama ni mtu wa kutukuzwa hvi
 
Back
Top Bottom