Naomba msaada wa haraka kwa mwenye mapenzi mema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa haraka kwa mwenye mapenzi mema

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mabreka, Aug 29, 2012.

 1. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana jf,

  Mimi ni ME 30's yrs, nimekuwa nikisaka mchumba/mke kwa muda mrefu sana bila mafanikio mpaka nikafikia kiasi cha kukata tamaa ya kuoa.
  Nimekuwa na bahati mbaya kila nikipata rafiki wa kike anakuwa yupo nje kabisa ya sifa za mwanamke ninaetamani kuwa nae.

  Miezi 3 iliyopita nilibahatika kupata kazi katika kampun fulan hapa dar, Ikiwa km bahati niliajiriwa na dada 1 so tukawa tumeripoti kwa siku moja.

  tulikumbukana coz tulikutana kwenye intvyu, so tukawa tunatambulishwa sehem mbalimbali za kampuni tukiwa pamoja. Kwa kuwa wote tulikuwa wagen na tumeajiriwa kwenye kampun 1 na depart 1 so ikawa kila mahali tunakuwa tupo pamoja (break fast, lunch) kuanzia asbh mpaka muda wa kufunga ofc.

  Imefikia point mpaka kila mtu kwenye kampuni anajua/ anafikiri kuwa sisi ni wachumba. Wengine wanahoji tunatarajia kufunga ndoa lini? hii imekuwa inanipa moyo kuwa tunaendana na tunaweza kuwa mme na mke.  Huyu dada nikamwona ana vigezo vyote ambavyo nilitaman mke/mchumba wangu awe navyo.(Huyu dada kwa utashi wangu inaelekea hana mtu, au kama yupo hawapo seriaz sana). So ninampenda kweli ila sijamwambia nikawa navuta kasi kwanza ili nijiridhishe kisaikolojia kuwa ni kweli nampenda kwa moyo wote na sio kama nimemtan.

  Siku zilivyokwenda nimegundua kasoro 1 ambayo huyu mrembo anayo ambayo inanisumbua akili yangu mpaka nashindwa kujua nifanye nini, nisonge mbele au nijipange upya kuendelea kusaka mke.

  Huyu dada anaghubu (Analalamika sana) na kugombana na watu hovyo bila hata sababu za msingi. Sehem ambapo huwa tunapata brek fast keshagombana na wahudumu wote, sehem ya lunchi hivyo hivyo.
  Anaonekana ana matusi ya rejareja sana, hajawahi kunitukana mimi ila niliwahi kumsikia anamtukana mtu kwenye sim matusi ya nguoni kisa kam beep. mazungumzo yalikuwa hivi:-

  mchumba: hallow
  aliebeep:hallow,
  aliebeep: wewe nani?
  mchumba: kwan umembeep mtu usie mjua?
  aliebeep: nimepewa no na jiran yako.
  mchumba:******* ,****,****, (matusi)?!!!!

  Nilishtuka baadae akaniomba msamaha kwa maneno yake machafu.

  Kuna wakati mwingine anakuja job akiwa hataki kuongea na mtu yeyote anasema yupo Upset (hana mood). nikimuuliza kulikon anajibu "haikuhusu".

  Sasa nikimtamkia kuwa napenda na akakubali si atanitesa sana ukizingatia mie sio mtu wa ugomvi na mopole sana?

  Moyo wangu unasita, tafadhali naomben mitazamo yenu.
  hope huku kuna watu wenye uzoefu na walishakutana na situation kama hii.
  asanten.
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,680
  Trophy Points: 280
  Dah!Kijana una kazi na uchaguzi wako,utadhani unataka kununua gari!Ngoja waje mi namalizana na huyu mama ntilie kwanza!
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Siku zote mimi nakataliana sana na watu wanaodhani mapenzi ni kati ya wawilit tu... Kama ni u hawara na urafiki wa mda yaani mko kwa ajili ya mahusiano ya bila future then huyo dada atakufaa. Unapo oa mke, huoi tu mwanamke ambae anakufurahisha roho na kukutuliza nafsi yako na mwili wako. Unaoa mtu ambae anapaswa kufaa kuwa rafiki, mshauri, mama mwema wa watoto wako na kiongozi bora wa nyumba yako to make it a home...

  Hapo umejuana naye ni mda mfupi, namuona hana simile, hana aibu wala hana ustaarabu... Sifa ambazo ni msingi sana kwa mtu ambae anastahili kuwa mke. Angekuwa na hizo sifa asingegombana na hao watu kazini - naomba tu imagine kuwa huyo dada hao watu ni baki, basi jua kwa kiasi kikubwa ndugu zako (na hata wa kwake) nawa treat hivo.

  Kutafuta mchumba vijana wengi sana wanakosea siku hizi (iwe wake kwa waume); Mnataka kuwa ikifika age ndio utafute mtu wa kuwa mke wako... Hio haistahili mara nyingi sana unaangukia garasha na kumbuka kuwa ukisha oa/oana ni for life. Hata hivo mie naona hujachelewa bado upo young... Cha msingi jipatie walau mwaka ama miwili kutafuta mwanamke ambae kweli anastahili kuwa mke na your life patner, Na sio kwa staili ambayo unatumia... Umekutana na mtu kazi siku chache tayari ukafikiria kutangaza ndoa...

  Nakutakia kila la kheri katika kumpta mke alie bora na familia iliyo barikiwa. Pamoja saana.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  hata wewe mtoa mada una gubu pia.

  Kukutana na mtoto wa watu ushaanza kumchambua na kuja kulalamika hapa kabla hata hujamwambia nia yako??

  Inaelekea wewe ni 'mdonho', unachambua sana, wewe ni 'perfect'??

  Halafu kingine, sina hakika kama unampenda huyu, au ni ile kiu yako ya kuwa na mpenzi hatimaye kuoa inakufanya unadhani unempenda huyu binti.

  Tulia kwanza, jua unachotaka na uachane mambo ya kukimbizana na umri kama feri la kigamboni.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Ati kama anatafuta gari, tena la mkopo! Kazi kweli!
  Siku atamsasambua mamako mzazi urudi tukushauri. Learn how to trust ur guts, dude!
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,680
  Trophy Points: 280
  Huyu kijana sijui vp,mke ni mtu muhimu sana,tatizo tunachukulia poa sana!Enwei,nimechoka kuandika,kwanza simu inaisha chaji,hebu msome dada AshaDii,itakusaidia!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nashukuru kwa ushauri wako mkuu.

  hapo kwenye red, mie hata kumtokea bado, ndo nilikuwa najipanga kumtokea ndo nikakutana na hayo majimambo
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  haya ndio 'mabreka' kwa kweli lol
   
 9. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye red, mie nimesoma shule za kata sijaelewa.

  Nashukuru kwa ushauri wako Kongosho, mie umri sio issue sijapata hofu kuwa nimechelewa.

  Hakuna alie perfect, ila sina ghubu, matusi, ila inawezeka nina udhaifu mwingine.

  Mie sipendagi matusi ndo maana moyo unasita.
   
 10. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkuu nimecheka mpaka nimevunjika mbavu!!!

  mawazo yako ni mhimu sana mkuu tia hata neno moja tu
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  Kuna msemo wa Kiingereza unasema
  'do no cross the bridge until you come to it'

  so wewe ulipaswa kuanza nae tu taratibu
  mkishindwana basi
   
 12. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sasa unanishauri ya nifunge macho nibebe jumla jumla?
   
 13. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkuu hapa unajua tupo ofic moja, kila wakati tunakuwa tunaona
  sasa mie naona ofc itakuja kuwa chungu km nitamtokea akakubali alaf baadae tuka uvunja urafiki/uchumba
   
 14. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mimi naomba kupingana na hoja kwamba mke ni wa wote..mke ni wa kwako na kama wewe unamfurahia ndugu zako watamfurahia tu na hata hawamfurahii sio big deal pia kumbuka wewe ndiye utakaa naye muda mrefu. Kama unadhani anafit kwenye vigezo vingi binafsi nadhani hilo la gubu na matusi linarekebishika.

  Ndio maana ya kukaa uchumba na bahati nzuri umeyaona haya mapungufu..Jaribu kutumia hiki kipindi cha uchumba kumrekebisha/kurekebishana na pia usidhani utampata mkamilifu kama yule wa gfsonwin . Wewe endelea naye taratibu na hayo mengine yanaweza kujiset..ndoa ni shule na wanafunzi ni wanandoa na hakuna anayeingia shuleni anajua kila kitu..mtajifunza mengine huko huko mbele ya safari

  Kila kheri ndugu!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu mpaka nimekuja huku jua ninaheshimu michango ya hapa.

  ila uamuzi wa mwisho upo kwangu hapa najaribu kuangalia mitazamo ya watu kuhusu hii issue.
   
 16. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkuu nashukuru kwa ushauri wako. Nitaufanyia kazi.
  hapo kwenye red umenivusha darasa mkuu, hata kumtokea bado sijamtokea ila nipo nae karibu sana kiasi kwaba nahisi hawezi kunikataa, ila lolote laweza tokea.
   
 17. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145

  ni kweli mtazamo wako kuwa ndoa ni yako kama umempenda wewe wengine hawana nafasi ya kukushauri hata kama unapotea.


  mimi sijaoa wala sina mpango, jamaa kagungua matatizo ambayo anadhani hatayaweza, ila vijana tulio wengi tunadhani kwamba kama mtu ana tabia ambazo zinakukwaza ATABADILIKA MKIOANA, hiyo mi napingana nayo 100% haiwezekani ashindwe kuficha makucha huku nje afiche akiwa ameolewa, nahisi atatukana mpaka wakwe.

  halafu umesema eti, MAMBO MENGINE YATAKUJA MBELE YA SAFARI. nani kakudanganya?

  kwa mtazamo wangu, ushauri watu wanatoa ila mwenye maamuzi ya mwisho ni yeye muhusika kunyoa au kusuka
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  afu kingine mabreka dansi

  acha kufikiria watu watakuonaje, wakati wewe uhusioano wako na huyo dada unavunjika (siombei iwe hivyo) na watu wakawa wanakusema, saa hizo labda kuna wafanya kazi wenzio wanauza viungo vya binadamu ili wafanikiwe. Nani hapa ana aibu kubwa moyoni mwake?? Hakuna la ajabu kihivyo.

  Nashukuru sikupewa moyo wa kuwaza wengine wananifikiriaje hasa wasionihusu, huwa najali hisia zangu na ninaowajali hasa kwenye mahusiano.

  Unadhani nyie ndio mtakuwa wa kwanza kuachana maofisini???

  Hebu fanyia kazi 'confidence' yako pia.

  Hata hiyo watu kuwaona pamoja na kuwauliza mnaoana lini, inawezekana ndio linalokuwehusha kwa huyo dada. Sina hakina na hisia zako kama ziko clear ndio nachojaribu kusema.
   
 19. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Sasa mdogo wangu hujaoa halaf bado unaniambia nani kakudanganya..huu uzoefu unautoa wapi??
  Sijakataa mtu kubadilika akiwa kwenye ndoa au kabla..but lazima ufahamu kuwa ndoa nayo ina mambo yaliyomo ndani yake..Sio kanuni kuwa mtu akiwa na tabia fulani akiingia kwenye ndoa basi huwa hazibadiliki..tumeona watu walikuwa makahaba na wameolewa wamebadilika pia..kwa hiyo hakuna kinachoshindikana bwana!!
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  MwEeh! Kwani wewe umeanza kazi tu hapo 3 months ago already unawaza kustaafu hapo hapo? Vijana wa siku hizi mnawaza kama kina Nyerere!
   
Loading...