Naomba msaada wa dawa ya jino napata tabu wakuu...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Wakuu naomba msaada kwa mtu anayefahamu dawa ya meno yanayouma napata tabu sana,nimekwisha ng'oa kama matatu hv sasa sitamani kutoa mengine...naomba msaada hasa dawa za asili....
 
MAUMIVU YA MENO.
( TOOTHACHE.)
i. Asali na mdalasini.

  • mdalasini kijiko 1 cha chai.

  • asali vijiko 5 vya chai.
Matumizi:
changanya na paka kwenye jino liumalo fanya hivi mara 3 kila siku hadi jino liache kuuma. ii. Asali na mdalasini.

  • asali kijiko 1 cha chai.
  • mdalasini kijiko 1 cha chai.
Matumizi:
changaya kwenye maji ya moto kisha sukutua kila asubuhi hii piahusaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomo.
 
Sera ya dawa ya jino kung'oa imepitwa na wakati. Siku hizi kuna tekinolojia ya Root canaly ambayo inahusisha kuua mishipa ya damu kwenuye jino, hasa lililotoboka sana kisha kuliziba kwa amalgum.

Kuna jino ambalo lilinisumbua sana 2004 nikatamani kuling'oa, kwanza niliziba mwaka huo, nikaendelea kugonga Pope Cone kama kawa, baada ya miaka mitano amalgum ilitoka, nikapiga root canaly mpaka kesho nagongea nyama choma.

Huduma hii inapatikana Muhimbili tena kwa bei rahisi. Fanya uchunguzi inawezekana kuna hospitali competent zaidi.

Angalizi.

Kuna tooth fills zingine zina madini yenye sumu.
 
Konyagi ya chupa ndogo...weka vifuniko vitatu mdomoni sukutua for a while tema au mema fanya 3 tyms a day na utakua poa...kinachofuata ni kua na utaratibu wa kupiga mswaki mara kwa mara na kuhakikisha unabadili mswaki kila baada ya wiki na ununue dawa genuine sio zile za kutembezwa na wamachinga ama madukani ambako zinaharibiwa na joto..nenda phamarcy kubwa au hata shopyte ama game
 
Kwa yule mwenye matatizo ya jino(kuuma), pokea maelezo yafuatayo kwa uwezo wa mwenyezi mungu litapoa.

MATAYARISHO
Chukua majani ya mtunda(muarubaini),majani ya mpera na magome ya muembe.Tia kwenye sufuria kisha chemsha kwa maji yaliyo safi kwa muda wa dakika 15 hadi 20.
Kisha chukua dafu kubwa lenye nyama, likate sehemu ya juu kwa lengo la kutengeneza mlango mdogo.Yatoe maji yote ya dafu kwa vile hayahitajiki na bakisha nyama tu.

MATUMIZI
Chukua maji yako ya dawa yaliyo moto na mimina kwenye dafu kiasi kwamba yakaribie kujaa.Kisha weka mdomo wako juu ya mdomo wa dafu kwa lengo la kuingiza mvuke wa dawa kwenye mdomo.Weka kisha ondosha kulingana na umoto wa maji ya dawa kwa muda wa dakika 3 hadi 5.
Kisha sukutua kwa maji ya dawa ambayo yameshapungua joto.
Endelea na zoezi hili asubuhi,mchana na jioni kwa muda wa siku tatu na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu utapoa.
 
Back
Top Bottom