Naomba msaada wa biashara ya kufanya

Naomba msaada wa biashara ya kufanya

vee vivian

Member
Joined
Jul 4, 2020
Posts
25
Reaction score
86
Habari wanajamii

Mnakumbuka nilileta changamoto yangu na hamkusita kunishauri vyema na sasa ule ushauri mlionipa umezaa Matunda

Nawashukuru kwa kila mmoja wapo kwa kusoma story yangu na kutia chochote kitu Moyo ukapoa maana niliwaza mengi Sana kwa wakati ule Ila kubwa Zaidi nilijitahidi sana kutafuta kazi majumbani na nilifanikiwa kupata Kazi ya kufua Na kufanya Usafi. Mpaka sasa nina elf 35 na mtoto nimeshamlipia Ada elfu 15.

ilichonileta; toka juzi nimepata hii hela nachanganyikiwa na hizi biashara mbili naombeni mwenye mwongozo anipe au mtazamo biashara nifanye ipi na jinsi kuanzia ya kwanza kuchukua Matunda Mabibo na kuzungusha mitaaani yaani kuchukua parachichi, chugwa, ndizi, tikiti, na yapili Ni kuchukua viungo vya mboga mabibo mfano nyanya, vitunguu ,hoho ,karoti ,bamia ,nyanyachungu, nazo nizunguzhe mitaaani ili mtaji wangu usife nanipate ata atleast yakuweka Kwa kibubu

Sasa toka juzi nawaza Sana nashindwa nifanye maamuz Gani naombeni msaada wa mawazo kati ya hizo biashara ipini nzuri kwa walaji ambayo nitaifanya Na utanipa wateja asanteni sana...mawazo Yenu ndo yataniongoza Tena Na Tena ..nafatilia comment
 
Hongera kwa hatua uliyofikia mkuu.
ushauri utakaopewa wateja wako wa kwanza wa uhakika ni hao unaowafulia. Kila la heri.
 
uza matunda tena kama unaweza jaribu sehemu kama karikoo unakua unatembeza madukani mchana unapita kwa mamantilie wakati watu wananua chakula unawauzia ila Nyanya sikushauri ni rahisi sana kuoza asa zikibaki kwa uwo mtaji unaweza kupoteza
 
Hongera kwa jitihada,sikiliza moyo wako japo hiyo ya nyanya,vitunguu naona ina wigo mpana wa wateja
 
Kama mjini matunda, mtaani kwako nyanya na mbogamboga, zingatia eneo lako mkuu ndo uamue na angalia uhitaji kama uko karibu na shule ata visheti, mihogo, ubuyu kamtaji kakikua wakaangie dagaa na samaki

Kila la kher
 
Kwanini usifungue genge?
Kuzunguka nakuonea huruma🥺
mtaji wake ni mdogo azunguke tu kwanza inaweza kumfungulia fursa nyingine asa aki target maeneo yaliokua kibiashara kama kkoo kama ana kichwa chepesi anaweza akaza kujifunza biashara nyingine wakati anauza ayo ayo matunda
 
Iyo pesa chukua kidogo unga wa ubuyu kilo.

Chukua vifungashio.

Tengeneza barafu gandisha kwenye freezer ata la butchani.

Uzia watoto washule, vinapewa sana pesa siku hizi
 
Back
Top Bottom