Kila ninapowasha simu (Nokia E61i) inaonyesha kuna installation inaendelea "Installing....". Baada ya kama dakika moja naletewa ujumbe "Unable to install the remaing part from memory card, to install the emaing part go to App. Manager"
nimekwenda App. Manager nakuta kuna App. moja, 20000480.sis, Not Installed, kila angalau kujaribu ku-install naambiwa "File corrupted". Hii app. siijui (nahisi ni kirusi) pia hakuna pendekezo la kuiondoa (remove).
Nimetumia mbinu kadhaa ikiwamo kuzima na kuwasha simu, soft formating, hard formatting, na ku-instakll upya Operating System, ila sijapata mafanikio yoyote.
Hivyo, naomba msaada wako wa kuindoa hiyo app. Siku njema, amani iwe kwako.