Ahsante Chief-Mkwawaangalia mambo haya
1.signal
huwa kikawaida 3g inakula chaji kidogo kuliko 2g, lakini kiuhalisia 3g inakula zaidi chaji kuliko 2g hii inatokana na sababu muda wote 3g inasearch network mpaka bar iwe full
hivyo angalia eneo lako voda wana network full? Airtel network signal zake ni ndogo? hili huwenda ndio tatizo
2. Aina ya 3g inayotumika
kikawaida mitandao yetu wana 3g za aina tatu
-wcdma/UMTS (3g)
-hspa (3.5g)
-hspa+(3.75g)
wcdma yenyewe ndio ipo slow na haili chaji sana na hspa/hspa+ ina speed ila chaji inaenda sana hivyo mitandao ya simu hutumia wcdma kama standby kutunza chaji pale usipotumia internet inaswitch kuja wcdma.
mitandao mengine haina wcdma kabisa muda wote ni h+ (hspa+) hivyo kusababisha simu kuisha chaji mapema.
hivyo angalia Airtel yako kama muda wote ipo H+
3. kuwasha gps
kuna watu wengi humu jukwaani wanalalamika wakieka line za Airtel gps inajiwasha, gps inakula sana chaji hivyo angalia na ya kwako kama inajiwasha