Naomba msaada mtoto wangu anasumbuliwa na tumbo

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,002
2,272
Madaktari wa JF habari zenu?

Naomba msada wa Hili. Katoto kangu ka miaka 5 kanaumwa tumbo tangia juzi juma pili jioni. Alianza kulalamika tumbo linamuuma hadi kulia halafu akawa ana joto kali sana la mwili. Pia alikuwa anaharisha Haja kubwa yenye milenda milenda yenye harufu kali sana. Wakati mwingine Haja kubwa ilikuwa inatoka bila control na anashindwa kuizuia sababu ya wepesi wa Haja yenyewe. Badae akalalamika kichwa kinamuuma sana.

Dawa alizotumia so far:
Alipata cephalexin suspension 10mls daily kwa ajili ya infection
Akapatiwa paracetamol kwa ajili ya kushusha homa
Akapatiwa na dawa Mseto ya malaria 2 Mara 2 (dozi ya mtoto).

Baada ya kutumia hizi dawa japo hajamaliza:
Halalamiki sana kuumwa kichwa
Homa pia imepungua sana (joto linapanda kidogo sana)
Na kuharisha choo chenye harufu kali kumeisha japo choo ni kilaini na bado kina milenda.

Kwanini nimewaomba ushauri:
Bado anajisaidia milenda ya rangi ya kijani na njano ambayo kila anapojiskia kujisaidia tumbo linakamua kwa maumivu makali sana sana na hiyo Haja yenye milenda haitoki haraka hadi analia. Pia Hali hii hujitokeza kila anapokula chochote hata Kama ni maji.

Wakuu naomba mnisaidie maana nimestaki.

Nimesafiri kijijini ambapo huduma za afya sio Kama mjini.

Natanguliza shukrani zangu kwa mtakaoguswa kunishauri.
 
Chukua sample ya choo kikubwa uende nacho hospitali, pia mpeleke mtoto hospitali kubwa emergency. Wakati unafanya hayo, mpe maji hata anywe kidogo lakini kila baada ya dakika kumi ana sip.
 
Asante, Ila tumesafiri tuko mbali na hospitali kubwa hapa zipo dispensary tu Tena za kisanii. Ndo maana nimeomba ushauri hapa. Ngoja nichek kesho km Hali ikiendelea keshokutwa turudi town
 
Madaktari wa JF habari zenu?

Naomba msada wa Hili. Katoto kangu ka miaka 5 kanaumwa tumbo tangia juzi juma pili jioni. Alianza kulalamika tumbo linamuuma hadi kulia halafu akawa ana joto kali sana la mwili. Pia alikuwa anaharisha Haja kubwa yenye milenda milenda yenye harufu kali sana. Wakati mwingine Haja kubwa ilikuwa inatoka bila control na anashindwa kuizuia sababu ya wepesi wa Haja yenyewe. Badae akalalamika kichwa kinamuuma sana.

Dawa alizotumia so far:
Alipata cephalexin suspension 10mls daily kwa ajili ya infection
Akapatiwa paracetamol kwa ajili ya kushusha homa
Akapatiwa na dawa Mseto ya malaria 2 Mara 2 (dozi ya mtoto).

Baada ya kutumia hizi dawa japo hajamaliza:
Halalamiki sana kuumwa kichwa
Homa pia imepungua sana (joto linapanda kidogo sana)
Na kuharisha choo chenye harufu kali kumeisha japo choo ni kilaini na bado kina milenda.

Kwanini nimewaomba ushauri:
Bado anajisaidia milenda ya rangi ya kijani na njano ambayo kila anapojiskia kujisaidia tumbo linakamua kwa maumivu makali sana sana na hiyo Haja yenye milenda haitoki haraka hadi analia. Pia Hali hii hujitokeza kila anapokula chochote hata Kama ni maji.

Wakuu naomba mnisaidie maana nimestaki.

Nimesafiri kijijini ambapo huduma za afya sio Kama mjini.

Natanguliza shukrani zangu kwa mtakaoguswa kunishauri.

Nimechelewa kuona ila hiyo ilikuwa Amoeba

Next time uongezee na metronidazole
 
Asante mkuu.

Japo Hali ilikaa ikatulia Labda tu nimpatie hiyo flagyl Kwa uhakika zaidi.
Alifanya exray 2 za tumbo (maeneo ya tumbo mawili tofauti) na ultra sound zote zikawa safi.
 
Hapana hamna haja, labda upime kwanza Choo chake
 
Back
Top Bottom