Naomba Msaada, mekosa ada laki tatu

0762713479

Member
Oct 10, 2017
8
1
Mimi ni mwanafunzi katika chuo cha ualimu Tabora mwaka wa kwanza ila nimekosa ada laki tatu. Nilikuwa nadaiwa laki tano ila nimeangaika mtaani nikapata laki mbili. Nisaidieni jamani maana hali mbaya hapa chuoni.
 
Utaambiwa hapa ni stori tu,kula ni kwenu..ungeweka maelezo ya kina ni kwa nini usaidiwe
 
Nimekoswa ada apa nimelipa laki mbili nimeambiwa huwez kusajiliwa adi nilipe hela yote nimekuja Jana chuo kutokea ukerewe please Wana jf nisaidieni
 
Mimi ni kijana

KIJANA pole sana kwa tatizo lako, linawakumba wengi sana....nakuombea upate hitaji hilo, ila nikuongezee na ushauri pia kwamba endapo haitapatikana kwa muda basi tumia option ya kuandika barua kwa Mshauri wa wanafunzi (Dean of Students) hapo chuoni kueleza tatizo lako wataona namna ya kukusaidia kwa kukupa muda zaidi wa kuendelea kuitafuta huku ukiendelea na masomo yako.....manake najua ili uweze kusajili masomo (course) zako kwenye academic system sharti uwe umelipa ada ya semister husika, ila kwa special cases, basi Dean anaweza kukupa barua ya waiver ukapewa acccess ya kusajili kozi na kuendelea na masomo ila kwa masharti ya kuclear ada hiyo kabla ya final exam za semister hiyo husika.
 
Kwa kuwa umeweka namba yako ya simu hapo ina maana hakuna siri, kwa hiyo ili usaidiwe fanya yafuatayo...
1. Wasiliana na moderator kuhusu hitaji lako.
2. Weka details zako pamoja na jina la chuo, namba ya usajili na account ya kudeposit hiyo ada (hakikisha ni account ya chuo si yako binafsi).
3. Endelea kutafuta msaada sehemu mbalimbali, by the way utaishije chuo bila hela ya kujikimu?
 
Weka maelezo zaidi,maana kuandika tu bila ushahidi haitasaidia mkuu
 
Mimi ni mwanafunzi katika chuo cha ualimu tabora mwaka wa kwanza ila nmekoswa ada laki tatu. Nilikuwa nadaiwa laki tano ila nimeangaika mtaani nikapata laki mbili. Nisaidieni jamani maana hali mbaya apa chuoni
omba shamba shule ulime mboga mboga uuze ulipe ada. mi nitakuchangia hela ya pembejeo. sio vizuri kuomba samaki omba ujuzi na nyavu ili uvue samaki vizuri.
 
Usipofanikiwa mitandaoni,mwandikie mkuu wa mkoa unakotoka,ama ufike ofsini kwake,uwe na details za kutosha,isije kuwa umekula hela ya wazazi halafu ukakimbilia jf
 
Mimi ni mwanafunzi katika chuo cha ualimu tabora mwaka wa kwanza ila nmekoswa ada laki tatu. Nilikuwa nadaiwa laki tano ila nimeangaika mtaani nikapata laki mbili. Nisaidieni jamani maana hali mbaya apa chuoni
Nilipitia hali kama yako pia. Nilichofanya

Nilikuwa nadaiwa Tsh 200,000 bila hiyo sifanyi UE

Nikaongea na marafiki zangu wanne ambao ni waajiriwa ili kila mtu anikope Tsh 50,000 maana mtu mmoja tu kukupa Tsh 200,000 cash ni ngumu.

Watatu wakanipa Tsh 50,000 kila mmoja, mwingine akanipa Tsh 30,000

Nikalipa, nika GRADUATE !
 
Back
Top Bottom