Pole sana. Ulianza lini? Hizi dawa ni wengi wanalalamika kuwa siku za mwanzo mwanzo zinaleta maluelue sana. Wengine wanasema wanaota ndoto mbaya na kila aina ya ghasia. Ila kadiri unavyotumia ndivyo dalili zinavyopungua na mwishowe unazoea. Mimi nakushauri ni vizuri urudi kwa daktari pengine anaweza kutoa jibu kamili baada ya kukuona au kukupima. Kila mtu huwa ana-react kivyake anapotumia dawa fulani na ni vigumu kupata ushauri wa kusaidia bila kumwona mtaalam ana kwa ana.