Vizuri umeuliza swali la msingi.
Huu ni ugonjwa vigumu kutambulika kirahisi, kwa vile hata mgonjwa huwa hajielewi na ni wale wa karibu naye sana wanaweza kumtambua.
Hata ukitambulikana mtu anajinyanyapaa na kuukataa hadi aonane na daktari mtaalam. Mgonjwa anaonyesha dalili za kuwa mkali wakati wote, hapendi utani, na hata kwa mambo madogo anaweza kuwaka hadi watu wanashangaa. Mtu anaweza kununa hadi wiki nzima.
Hali ikiwa mbaya bila kujielewa vitu vyake anachana chana au kuvigawa akiamini anafanya usafi. Nina ndugu wa karibu alikuwa akifanya hivyo na tulifanya jitihada za ziada kumpeleka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya akili. Ni miaka zaidi ya 8 sasa ndugu yetu anapata vidonge vya Oleanz ambavyo pamoja na sindano za mwezi huwezi kujua kabisa kuwa ana tatizo.
Kutokana na mabadiliko ya kimaisha watu wengi wanaugua ugonjwa huu.