Naomba mrejesho kwa aliewahi kuagiza Alibaba

Oct 14, 2015
6
12
Kuna hii website www.alibaba.com wana bidhaa nyingi kutoka China kuanzia electronics mpaka nguo. Nilikua nauliza kuna mtu yoyote alishafanya nao kazi? Yaani aliagiza bidhaa akiwa hapa TZ akaletewa? Nisije kutuma hela zangu bure ziliwe kwa sababu cyber crimes zimeshamiri now days...

Nawasilisha
 
Mkuu kama unataka bidhaa hapo ndio upo salama kuliko sehemu ingine. We agiza watakuletea bila shaka yoyote si wezi hao. Usijicheleweshe kwa maneno ya watu nilishaagiza bidhaa nyingi sana na hao jamaa.
 
Kuna hii website Manufacturers, Suppliers, Exporters & Importers from the world's largest online B2B marketplace-Alibaba.com wana bidhaa nyingi kutoka China kuanzia electronics mpaka nguo. Nilikua nauliza kuna mtu yoyote alishafanya nao kazi? Yaani aliagiza bidhaa akiwa hapa TZ akaletewa? Nisije kutuma hela zangu bure ziliwe kwa sababu cyber crimes zimeshamiri now days...

Nawasilisha

Ni kampuni genuine, haina tatizo. Fuata tu masharti yao, usimlipe supplier moja kwa moja bila kupitia kwao.
 
alibaba sio wafanyabiashara ni sehem tu kama e bay.. ambapo wafanya biashara tofaut wanakutana kuuza bidhaaaa zao..

so wapo wafanyabiashara waaaminifu na wapo na matapeli pia..

nina jamaa yangu ameshapigwa usd 2000 na supplier mwizi.. hakutuma mzigo kabisa.. japokuwa ni mzoefu ameshaaagiza sana huko alibaba na mizigo akaipata
 
Khaa!! Alibaba ni safe tu. kwanza unaweza kuanza kuagiza kwa kupitia kwao kwani supplier halipwi pesa hadi uwahakikishie mzigo wako umeupata ukiwa ndiyo ulivyouagiza. Ukizoeana na suppliers unaweza kuagiza moja kwa moja kutoka kwao na bei itashuka. Anza kwanza kupitia Alibaba ni salama na pesa yako inaweza kurudishwa kama usipopata mzigo wako. Kuna jamaa anafanya hivyo mara nyingi na hajawahi kulalamika.
Dunia Kijiji
 
Utapata mzigo wako wala sio matapeli ila kumbuka bidhaa sio za alibaba ni za watu binafsi, pia vitu vingi vya pale ni low quality
 
alibaba sio wafanyabiashara ni sehem tu kama e bay.. ambapo wafanya biashara tofaut wanakutana kuuza bidhaaaa zao..

so wapo wafanyabiashara waaaminifu na wapo na matapeli pia..

nina jamaa yangu ameshapigwa usd 2000 na supplier mwizi.. hakutuma mzigo kabisa.. japokuwa ni mzoefu ameshaaagiza sana huko alibaba na mizigo akaipata

Mzoefu Alibaba hawezi kupigwa!!! Kwa sababu kwanza humlipi supplier, unawakabidhi pesa zako Alibaba mpaka unapopokea bill of lading kutoka kwa supplier ndio unawapa go ahead wamlipe supplier.
 
Jaman nimeitafuta hii thread baada ya kuwa na uhitaji wa kuagiza mizigo kupitia alibaba, kwamaana hana mawakala bongo ni online kwa online??
 
Khaa!! Alibaba ni safe tu. kwanza unaweza kuanza kuagiza kwa kupitia kwao kwani supplier halipwi pesa hadi uwahakikishie mzigo wako umeupata ukiwa ndiyo ulivyouagiza. Ukizoeana na suppliers unaweza kuagiza moja kwa moja kutoka kwao na bei itashuka. Anza kwanza kupitia Alibaba ni salama na pesa yako inaweza kurudishwa kama usipopata mzigo wako. Kuna jamaa anafanya hivyo mara nyingi na hajawahi kulalamika.
Dunia Kijiji
Nielekeze kidogo hapo Boss
 
Back
Top Bottom