Naomba Mechi ya Yanga sc vs Mamelod iahirishwe

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,875
Baada ya kumsikiliza kocha wetu, mbabaishaji Miguel Gamond katika mkutano na waandishi wa habari, Nimejikuta nimekata matumaini ya timu Yangu kushinda mchezo wa kesho dhidi ya kabayelo masandawana.
Kocha anatoa sababu ambazo hazina mashiko, mara alikosa muda wa kuandaa timu, mara Aziz ki na Diarra hawajafika, yaan ilimradi ukajanja kajanja tu.

Ni wazi amekosa mbinu sahihi za kuwakabili hao wasouth Afrika, ukizingatia ubaridi na hofu aliyopata baada ya kushangaa kocha wa mamelod ametaja kikosi chote cha yanga hadi wachezaji wa akiba huku yeye akiwa hana alijualo kuhusu kina allende na toboho makoena, kwa kifupi jamaa ni kama anatafuta på kujifichia.

Nashauri viongozi wa Yanga waandike barua Leo hii CAF, waseme timu nzima imepata ugonjwa wa kuhara ili mechi iahirishwe la sivyo, tutakumbana na dhahama mbaya sana.

Nawasalisha
 
Mind game
1000021720.jpg
 
Baada ya kumsikiliza kocha wetu, mbabaishaji Miguel gamond katika mkutano na waandishi wa habari, Nimejikuta nimekata matumaini ya timu Yangu kushinda mchezo wa kesho dhidi ya kabayelo masandawana...
Wewe nenda uwanjani acha maneno mengi, auwezi kupewa Kila kitu vitani, yanga wapo vitani ivyo wenye akili kubwa tunajua kinachoendelea
 
Eti mind game...mind game kwa waafrica wenye kujua fitna za ngozi nyeusi...
Hahahahahhahaha
 
Mkuu Naona Ulikata Tamaa Kabisa Na Kumu-underestimate Grand Wizard Gamond Ila Tumecheza Vizuri Pamoja Na Kukosa Wachezaji Wetu Muhimu.

Kongore Kwa Grand Wizard Gamond.
 
Back
Top Bottom