Naomba maelezo kuhusu Recategorization kwenye suala la ajira

Naomba maelezo kuhusu Recategorization kwenye suala la ajira

Habari za muda huu wadau wa JamiiForums.

Naomba ushauri na maelezo kuhusu Recategorization kwenye swala la ajira.

Mimi ni Clinical Officer lakini pia ni Mwalimu wa mathematics Ngazi ya degree. Niliomba ajira za Ualimu degree (mathematics) na nimepangiwa post tayari.

Niliomba ajira hii baada ya account ya Ajira portal kuleta shida na kuninyima fursa ya kuomba utabibu.

Je Itawezekana Mimi kubadilisha kada ya Ajira kutoka education kwenda Afya kulingana vigezo nilivyoweka? Na itachukua muda Gani kufanya Recategorization kama Itawezekana?

Naombeni ushauri wadau.
Umeniwazisha tofaut leo.. Uliwezaje soma deploma afya after degree.. Naomba niinspae namimi aloo.. Io strength.. Pia ulisoma kwa hatua zpi.. Sorry lkn niko nje ya mada kdg
 
Umeniwazisha tofaut leo.. Uliwezaje soma deploma afya after degree.. Naomba niinspae namimi aloo.. Io strength.. Pia ulisoma kwa hatua zpi.. Sorry lkn niko nje ya mada kdg
Inawezekana. Ni kipato chako tu na calculation. Unataki nini maisha I mwako??

Ukiwà na courage , desire burning inside utaweza kusoma.
 
Mkuu
1. Nenda kwanza karipoti kituo cha kazi ulikopangiwa. Hii ni hatua muhimu sana ili uwe ni Mwajiriwa hai. Kumbuka wapo walioajiriwa na wakafariki kabla ya kuripoti Kituo cha kazi(duty station). Unataka udhaniwe hivo kwamba ww ni mmoja wapo?
2. Recategorization anafanyiwa Mwajiriwa aliye kazini Tayari lakini akaenda kusoma/kujiendeleza na amefuzu masomo yake. Kama hicho alichoenda kusomea ni katika Fani hiyo-hiyo ya awali utaweza kuomba kufanyiwa marekebisho ktk ngazi ya mshahara e.g. ulikuwa Dip. holder lakini sasa ww ni Deg. holder ktk fani hiyo. Utafanyiwa recategorization na ngazi ya mshahara itazingatia kwa anayeajiriwa mara ya kwanza bila kuangalia ulikuwa umefikia ngazi gani ya mshahara kipindi ukiwa na Dip. i.e ni kama unaanza moja.
Hii ya bila kuangalia ulifika ngazi gani ya Mshahara imefanya Washua wengi sana wakatae kusoma tena kabisaa
 
Back
Top Bottom