Naomba Lowassa uniweke sawa hapa Mzee wangu ninayekuheshimu

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Mzee wangu, heshima Nyingi kwako.. unakumbuka uliwahi kuniambia(sidhani kama uliwaambia Na wenzangu sina Hakika) kwamba Hutaki kwenda Ikulu damu ya Mtu ikimwagika.

Kwa kweli That time kwenye Uchaguzi, nchi ilikuwa imekunoga, kama kiberiti, ungewasha chaa kingelipuka kitu nchi nzima, lakini Kwa Busara Zako ukasema no, hapana kuandamana, hapana kufanya fujo, sitaki kwenda ikulu Kwa Damu ya Mtu kumwagika. Watu tukatii, tukatulia .. bara waliiba Kura ila Zanzibar sio kuiba tu Bali Kunyakua kimabavu mchana kweupe.. tukakaa kimya..

Sasa kulikoni UKUTA.. Ukuta huu si unaweza kumwaga Damu ambayo ulikataa isimwagike.. au kumwaga Damu kwenye UKUTA Ruksa ila kwenye kupigania matokeo ya sauti ya wengi Mwiko??..

Samahani Kwa kweli hapo tuu nipate ufafanuzi..

Brain yangu inashangaa vitu vingi, Kunji au maandamano huwa ni Hatua ya Mwisho Kabisa baada ya mistakabali yote ya mezani kugonga UKUTA. Kumbuka Mweshimiwa tumekuwa tukirukia tamati ya maamuzi ya Jazba kwenye kila kona. Mfano Bungeni, Bado kulikuwa Na mijadala ya kiutu kumaliza sintofahamu lakini tukarukia kufunga vinywa na kutoka nje tukimgomea binti mdogo wa miaka 39 tu ambaye alitakiwa kufunzwa na kuelekezwa.

Tumekuwa na maamuzi ya jazba ambayo sidhani kama yana Mantiki nyuma yake..ulipo kuja CHADEMA, niliamini sasa CHADEMA itasukwa itoke kwenye Uanaharakati kiwe chama kikomavu cha Siasa.. nguvu kubwa iliyoingia CHADEMA sasa itumike kujenga Chama kujiandaa kushika dola lakini naona tunarudia kwenye siasa za jazba na maandamano.. Nguvu kubwa iliyoingia CHADEMA tumeitelekeza, wengine haoo wanarudi walikotoka, Sisi tunaimba UKUTA.. UKUTA ndio Kujenga Chama?!?!tunaelekea WAPI MKUU.
 
Kuandamana ni haki ya kikatiba hivyo sioni tatizo! Hiyo damu unayoisema itamwagika atakaye imwaga ni polisi na si mtu mwingine, kwani wamesema wanaandamana kwenda kumwaga damu? Hivi Magu na serikali yake wanaogopa nini? Kama wewe ulifanikiwa kusoma kwenye vyuo vya tanzania lazma utakuwa ulishawahi kuandamana. Na maandamano hutokana na watu kudai haki yao.

Hivyo kukaa na kukubali kila kitu kinachosemwa kwa kisingizio cha kumwaga damu nadhan serikali ndio italaumiwa sio Lowasa wala mpinzani yeyeto. Hivi unajua kazi ya Polisi? Wao kwanini wasihakikishe hayo maandamano yanakuwa ya amani? Mara nyingi nguvu hutumika pale akili inapoacha kufanya kazi. Naona hii serikali hata akili kidogo waliyonayo hawataki kuitumia wao ni nguvu tu!

Ni kuulize swali mkuu! Hivi wazee wetu waliopigania uhuru kama wangekubali kila kitu kiende kama wazungu walivyotaka leo tungekuwa hapa? Wakati wa Kikwete kwani hao Ukawa si waliandamana? Kuna mifano ya viongozi wengi duniani walijaribu sana kutumia majeshi ili watekeleze sera zao za kidhalimu but nguvu ya umma ikisema basi ni basi, no one will stop it.

Ndugu zetu Albino waliuwawa na bado wanaishi maisha ya mashaka ila hakuna nguvu yoyote jeshi la polisi linatumia kuwalinda! Just imagine kama wangekuwa na nia ya kutokomeza mauaji ya albino kwa nguvu wanayotumia kupambana na upinzani leo hii ndugu zetu si wangekuwa na maisha ya raha kama wewe?
 
Sio maandamano ya kwenda ikulu ni maandamano ya kupinga udikteta Tanzania....halafu haya sio maamuzi ya mtu mmoja kama Bob bali ni maamuzi ya chama
maamuzi ya ufipa huwa hayana mashiko kwani opereshen zlkua nyingi,,, ukuta niwa kupingwa kila kona ,, mtaandamana wenyewe mstupgie kelele hapa sisi tunawaza maendeleo
 
Waandamanaji hawana silaha yoyote.Je hao polisi hayo mazoezi kama ya vita ni kwa ajili ya waandamanaji ambao hawana silaha yoyote mkononi?Ama kweli hii ndio Tanzania ambayo hatujui tunaelekea wapi.
 
huu ushauri ungewa ccm na mwenyekiti wao
kumpa lowassa ushauri huu ni sawa na kumvunjia heshima yake.
 
Sio maandamano ya kwenda ikulu ni maandamano ya kupinga udikteta Tanzania....halafu haya sio maamuzi ya mtu mmoja kama Bob bali ni maamuzi ya chama
Nitaandamana tu ikiwa nitamuona mbowe na mkewe, lowassa na mkewe pamoja na watoto wao wakiwa front line, nisipowaona sidanganyiki, sitakubali kuwa mbuzi wa kafara wala kuwa ngazi kwa wanasiasa wanaosaka umaarufu kupitia damu za watu.
 
Majibu yapo kwenye tovuti ya chama kama ilivyo kwa sera ya chama. Wale wakulima vijijini wakitaka kujua sera ya CDM wakasome kwenye tovuti. The teh teh
 
Mzee wangu, heshima Nyingi kwako.. unakumbuka uliwahi kuniambia(sidhani kama uliwaambia Na wenzangu sina Hakika) kwamba Hutaki kwenda Ikulu damu ya Mtu ikimwagika.

Kwa kweli That time kwenye Uchaguzi, nchi ilikuwa imekunoga, kama kiberiti, ungewasha chaa kingelipuka kitu nchi nzima, lakini Kwa Busara Zako ukasema no, hapana kuandamana, hapana kufanya fujo, sitaki kwenda ikulu Kwa Damu ya Mtu kumwagika. Watu tukatii, tukatulia .. bara waliiba Kura ila Zanzibar sio kuiba tu Bali Kunyakua kimabavu mchana kweupe.. tukakaa kimya..

Sasa kulikoni UKUTA.. Ukuta huu si unaweza kumwaga Damu ambayo ulikataa isimwagike.. au kumwaga Damu kwenye Ukuta Ruksa ila kwenye kupigania matokeo ya sauti ya wengi Mwiko??..

Samahani Kwa kweli hapo Tu nipate ufafanuzi..

Brain Yangu inashangaa vitu vingi, Kunji au maandamano huwa ni Hatua ya Mwisho Kabisa baada ya mistakabali yote ya mezani kugonga ukuta. kumbuka Mweshimiwa tumekuwa tukirukia Tamati ya maamuzi ya Jazba kwenye kila kona. mfano Bungeni, Bado kulikuwa Na mijadala ya kiutu kumaliza sintofahamu lakini tukarukia kufunga vinywa Na kutoka nje tukimgomea binti mdogo Wa miaka 39tu ambaye alitakiwa kufunzwa Na kuelekezwa.

Tumekuwa Na Maamuzi ya Jazba ambayo sidhani kama yana Mantiki nyuma yake..ulipo kuja CDM, niliamini sasa Chadema itasukwa itoke kwenye Uanaharakati kiwe chama kikomavu cha Siasa.. nguvu kubwa iliyoingia Chadema sasa itumike kujenga Chama kujiandaa kushika Dola lakini naona tunarudia kwenye Siasa za Jazba Na maandamano.. Nguvu kubwa iliyoingia Chadema tumeitelekeza, wengine haoo wanarudi walikotoka, Sisi tunaimba UKUTA.. Ukuta ndio Kujenga Chama?!?!tunaelekea WAPI MKUU.
umezungumza vyema, japo kuna mawazo yako wengine watayaona siyo ya maana lakini umeeandika jambo lenye mantiki kubwa ndani yake.
 
Pengine kuna njama za makusudi za kumfanya huyu mzee mwenzangu akose mvuto aliokuwa nao CCM, na kwa kweli ameshuka kwa kasi, na hii inaenda kumtoa kwenye ulingo wa kisiasa kabisa, rejea ile kauli ya alipo wapo, wameshamkimbia wengi tu. ALIPO HATUPO!!
 
UKUTA tutaandamana kwa amani kama sheria na katiba inavyosema
Tatizo ni kwamba, kuna watu wamepania kufanya yao siku hiyo ambapo wao si wanasiasa, ni watu wa kucheza na fursa zinapojitokeza!
 
Acheni Propaganda zenu za kitoto. Hivi wanaoisapoti Operesheni UKUTA ndiyo watamwaga damu ya wengine au wao ndiyo mpaka sasa wanatishiwa kumwagwa damu yao iwapo wataandamana? Yaani wanaojitayarisha kumwaga damu unawaacha kuwauliza unamuuliza mtu ambaye damu yake inawindwa imwagwe, Hii siyo sawa hata kidogo!!
 
hakuna maandamano ni njia ya kumstress magufuli na kumfanya awebusy na UKAWA kuliko kutimiza ahadi zake kwa wananchi. likiisha hili la UKUTA watakuja na lingine ili mradi tu kumpa stress na kuteka muda wa mh Raisi abaki akipambana na Chadema kuliko kutimiza ahadi zake. yaani cku anayokuja kushtuka miaka imeenda 2020 badala ya kusema nimetiza ahadi anaanza kutoa ahadi tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom