Naomba la level ngazi za mishahara

Naomba la level ngazi za mishahara

diso

Member
Joined
May 15, 2013
Posts
20
Reaction score
0
Wana JF naomba kufahamu hivi hizi mamlaka za maji level za mshahara kwa mtu wa degree zikoje?kwa mfano mtu alie ajiriwa Mwanza(mwauwasa),Dsm(dawasco)na mtu alie ajiriwa Songea(souwasa) wanaweza kuwa sawa.
 
Wana JF naomba kufahamu hivi hizi mamlaka za maji level za mshahara kwa mtu wa degree zikoje?kwa mfano mtu alie ajiriwa Mwanza(mwauwasa),Dsm(dawasco)na mtu alie ajiriwa Songea(souwasa) wanaweza kuwa sawa.
level na ngazi??????????????? mjmi bado sijakuelewa diso
 
Last edited by a moderator:
Samahani kwa makosa hayo naomba isomeke hivi "Naomba kufahamu ngazi za mishahara"

Naomba kuwakilisha... obama wa bongo
 
mishahara ya watumishi wa mamlaka za maji inatofautiana kutoka mamlaka moja hadi nyingine.
Unatakiwa ufahamu pia hizi mamlaka za maji zimegawanywa kimadaraja kuna daraja A,B,C
Mamlaka za daraja A kama sijakosea ni DAWASCO,ARUWASA,MWAUWASA,DUWASA na mamlaka ya Tanga na Songea hizi zinaitwa daraja A kwa sababu hizi zina mapato mengi ya kutosheleza kulipa mishahara ya watumishi pamoja na kulipia gharama zote za uendeshaji, Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hizi ndio wanapanga mishahara ya watumishi jinsi wenyewe watakavyoona na jinsi mapato ya mamlaka husika yanavyojitosheleza na kuomba kibali kutoka kwa katibu mkuu Utumishi na Msajili wa hazina ili waweze kulipa hiyo mishahara wanayoitaka wao.
Mishahara inatofautiana kwa kila mamlaka za daraja A.
Mamalaka za Daraja B ni nyingi kidogo sina data zake kamili,ila nyingi ni za miji midogo kama Singida,Kilimanjaro, etc hizi nazo zinaweza kulipia gharama za mishahara na baadhi ya gharama za uendeshaji,ila zinapata pia ruzuku kutoka serikalini,hizi nazo zinajipangia zenyewe viwango vya mishahara ila si mikubwa kutoka hizi mamlaka hata makusanyo yao sio makubwa, na
Mamlaka za Daraja c nyingi na mamaaka za maji za miji midogo kama ni zile Mamalaka ya maji mji mdogo himo ,Mamlaka hizi ni zile zote ambazo kwa kiasi kikubwa zinaendeshwa na fedha kutoka Serikalini Katika kulipa mishahara, watumishi wa mamlaka hizi wengi unakuta ni watumishi wa halmashauri ya wilaya ya sehemu husika au watumishi wa wizarani ya maji hivyo mishahara yao ni ya TGS inategemea sasa na cheo chake.
Kwa kifupi hakuna uniformity ya mishahara kwenye hizi mamlaka
 
Asante kwa maelezo mazuri nimepata uelewa sasa.
 
Back
Top Bottom