Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba

Hamadee

Member
Jul 24, 2011
6
4
HABARI WANAJAMVI, Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba za nguo mbalimbali hapa Tanzania na nje. Connection naomba na kwa ushauri pia nipo tayari kupokea kwasababu ndiyo nataka kuanza hii biashara
 
HABARI WANAJAMVI, Naomba kuuliza kuhusu chimbo zuri la kununua mitumba balo za mitumba za nguo mbalimbali hapa Tanzania na nje.
connection naomba na kwa ushauri pia nipo tayari kupokea kwasababu ndiyo nataka kuanza hii biashara
Nicheki whatsapp nitakuwa nakuagizia moja kwa moja kutoka Dubai.
+971527794329.
IMG-20220717-WA0009.jpg
 
Habari za muda huu wanajua ii. Gt na professionals wa mambo mbalimbali. Poleni Kwa kadhia, hasa wale wanaosumbuliwa na mapenzi, ajira na siasa. Niseme tu tuendelee kupambana, hamko peke yenu.

Nimeona Kuna uhitaji mkubwa wa watu kufahamu biashara ya mitumba kwani wengi wetu wamekuwa wanaulizia Mara Kwa mara na wengine kutoa baadhi ya wanachokijua kujibu maswali Kwa wasiojua. Nianze kwa kusema kwamba hili la majibu mafupi na uhitaji wa Kujua limenisukuma niandike haya.

Mitumba si biashara rahisi kama tunavyofikiria. Ina utaalamu mchache ambao ni Basic. Utaalamu huu ndio unanisukuma kuandika machache.

Kwanza kabisa, wauza mitumba wapo wa Aina nyingi. Kuna suppliers, ambao wananunua robota 20,10 au 50 Kwa wahindi na kuweka mzigo stoo na kuuza kwa WAFUNGUAJI. Kwa namna hiyo, mnyororo wa Belo unaweza kupita mikono zaid ya mitatu mpaka Belo kumfikia anaefungua Belo kuuza nguo Kwa wavaaji/wuazaji.

Mfunguaji (mfungua Belo) ni mfanya biashara ambae anaweza kuwa na mtaji Kati ya laki 5 (Belo 1/2 kutegemew na uzito au bei Husika) ambae anamiliki kizimba (sokoni n. K) anetegemea Sana kuuza nguo moja moja Kwa wateja wa Aina 3. Napendekeza ukiwa na mpango wa kufungua Belo wateja hawa uwe nao. Hapa nitazungumzia Mtumba grade 1.

1. Mteja wa JUMLA
Ni lazima ukubali kwamba, nguo za mitumba zinaweza kutoka Belo moja lakini ubora ukatofautiana. Kuna nguo unaweza kuuza Kwa elfu 10 (tisheti hii bei ni kubwa mno), Kwa jinzi (ukauza mpaka elf 30). Lakini Belo hilohilo litakupa nguo ambayo hata elfu 1 Mia tano huuzi. Hivyo kadri unavyouza lazima uwe na utambuzi wa bei halisi ya nguo iliyo mkononi. Usikatae kuuza elfu 10 ukaione nzur Sana ukaja kuiuza elfu 7 upate hela ya kula kwanza.Au kinyume chake, ukauza nguo elf 10 kumbe hata elfu 25 ungeuza.

MTEJA WA JUMLA NI YULE ANAEKUJA KWAKO KUNUNUA NGUO ZOTE ZILIZOBAKI MKONONI/KIZIMBANI MWAKO,ILI AKAZIUZE (HAWA MARA NYINGI WANA MWAGA CHINI AIDHA KANDO YA BARABARA AU MINADANI) . Mara nyingi Kwa tisheti wananunua bei ya jumla Kati ya 700 mpaka 1300 inategemea na mapatano.

2. MAWINGA (MAPOINTA)
Hawa pia ni wateja muhimu Sana unapofungua Belo. Ni viungo muhimu Sana kuchagua NGUO KALI kutoka kwenye Belo lako wakauze. Hawa huwa na tabia ya kuchagua Sana, kwenye nguo 300 katika Belo lako ni kawaida kupata nguo 3, 4 au 10 usiawchoke. Wanakuaga na "strong negotiation skills". Wasumbufu. Ila ni muhimu kwani wanasaidia Sana kukutoa kwenye msongo wa kutokuuza, mzigo mbaya au wanakubusti kurudisha mtaji kwani wanaoweza kusababisha ukarudisha nusu ya hela yako mapema mno. Kwa tisheti wengi wapo Nje ya jengo la CHINA PLAZA. Wanakuaga na MAGOLI yao. Kwa tisheti huwa wananunuaga Kati ya elf 5 mpaka 8.

PIA, MAPOINTA, wengine wanaitwaga MAWINGA hawa ni watu ambao hawanunui nguo kwako. Hawa wanaleta mteja kizimbani kwako na kuuza kama za kwao. Ni wazuri pia kuropoka bei. Tisheti ya elf 5 wanaoweza kumropokea mteja kuwa bei ni 12. Ni moja Kati ya watu wanaoharibu biashara za mitumba sokoni zinaonekana ghali. Karume na ilala wamejaa Sana hawa. Ni wa muhimu ila hutakiw kuwaamin, wanaoweza kukudhulumu au kuiba. Lakini pia, ikitokea unawaamini unaweza kuwapa nguo wakauze wakulete hela. Kuwajua pia kunahitajika apa. Wanakuaga na uwezo wa kuuza idadi nyingi ya nguo kuliko mwenye Mali yako. Very potential.

3. WAVAAJI
Hawa ni watu kam mimi na wewe. Ambao wanapita au wanvutiwa Kuja kununua. Hawa wanaoweza kuuziwa na wewe au mawinga. Mara nyingi huwa hatuwajali Sana sabab WANAPITA TU. tunaweza kubambika nguo zilizotoboka wasipoona. Ni biashara, ni rizki. Lakini pia wakijenga uaminifu na kurudi rudi huwa tunawachagulia saizi nzur/dizaini wanazopenda tunawtunzia au kuwapigia simu waje kuziona/ kununua.

Aina nyingine ya wauza mitumba ni hawa MAWINGA /MTUKATI /MAPOINTA. hawa Mara nyingi huwa wanachagua nguo chache NZURI TU. Wanakuaga na teknik za kuchagua nguo nzur Kwa JICHO LA MTEJA. hawa ndio ambao tunawakuta wamebeba nguo mkononi kando kando ya barabara au kukuleta majumbani wengine wanaposti mitandaoni (what's ap status, insta nk). Tabia yao kubwa ni kununua nguo nzur tu (Kam nlivyoeleza). Hawana mitaji mikubwa hawa hata elf 50 inawatoshaga. Pia muda mwingine wanalindwaga na uaminifu tu, wanapewa wakauze walete hela.

Aina ya mwisho ya wauza mitumba ni WAUZA JUMLA. Hawa jamaa huwa na kelele kweli kweli. Kokte wakikaaga hawa lazima kuwepo na kelele za kutangaza biashara yao. Hawa wanatumia hesabu za paukwa pakawa. Mfn. Wananunua tisheti bei ya jumla (nimewaeleza juu hapo Kam wanunuzi wa jumla) Kwa kiasi cha shilingi 800 au 900 Kwa tishet 1 kwa mana tishet 350 *900 (bei) = na Laki 4 mfano. Wanazobeba kwenda kuzimwaga chini na kunadisha elfu tatu 1 (ndani ya siku 2). Mfano umeuza tisheti 80 *3000= na Laki 3 na 20. Siku ya tatu unaanza kunadisha Kwa elfu mbili mbili na kuuza tisheti (260 zilizobaki). Unauza elf mbili-mbili tishet 100 (ndani ya siku 2) Sawa na laki tatu. Siku inayofata unaanza kuuza bukubuku. Tu nategemea kupata faida nyingi Kwa kadri tunavyoshusha bei kila siku Kwa sabb ya kulindwa na yile bei iliyoanza kutumika Mara ya kwanza kabisa. Ukisharudisha mtaji zinazobaki hata Mia tano-tano unauza tu.

NB: HAKUNA UWEZEKANO WA KUUZA TISHETI ZOTE.

HAWA WOTE WANAWEZA KUWA WAUZAJI WA JUMLA KULINGANA NA MASLAHI YAO. SAMAHININI KWA MUANDIKO MBOVU WENYE UHITAJI KARIBUNI HAPAHAPA JUKWAANI KWA KUTAKA UELEWA ZAIDI


UPDATE .
Robota utazipata Mnazi mmoja LUMUMBA na NARUNG"OMBE au NKRUMA STREET zilipo ofisi za LATRA. TBC KULE tazara kwernye kampuni moja inaitwa BAZAAR
 

Attachments

  • Screenshot_20220926_114737_com.whatsapp.w4b.jpg
    Screenshot_20220926_114737_com.whatsapp.w4b.jpg
    87.1 KB · Views: 148
nataka Cadet mtumba kali kali zile kwa sh elf 5 nitapata wapi mkuu Karume au ilala boma na mida gani mzuri wa kwenda?
Kadeti zinapatikana mkuu. Nenda ilala boma asubuhi Kati ya saa 1 mpaka 5 utapata. Kama unaweza kusimama kwenye mnada kugombea Kwa kupandisha dau. Au unaweza kufika sehem moja maarufu hapo panaitwa "Ashanti". Ukifikishwa Ashanti Muulizie mtu anaitwa Muba au Ostadhi SELE.

Hawa watu wawili wambie umepewa address na MJOMBA. Hao watakuuzia lakini elf 5 Kwa ubora wa ngu zao hawakuuzii. Ni bora uweke bei ya elf 8 (Standard) ambayo itakuruhusu uchague siku ANAYOFUNGUA.

NB. NI BORA UFIKE SIKU ANAYOFUNGUA BALO UPATE NGUO AMBAZO HAZIJACHAGULIWA SANA UKAUZE HARAKA KWA FAIDA NZURI.
 
Somo zuri sana bro. Mimi nina maswali machache.

1. Nikitaka kuanza biashara kwa kununua baro, la nguo, viatu na mabegi, nijipange na bei gani makadirio?

2. Nitaamini vipi kwamba ili baro ni quality? Niliambiwa yana bei tofauti tofauti.

3. Je, nitajuaje kama ilo baro limetoka nje (ulaya) isije kua kuna wahuni wanayafunga hapo hapo karume au Kariakoo wanatupiga sisi wageni ila quality wanauziana wanaojuana tu.

cc Sir Midabwada
 
Kadeti zinapatikana mkuu. Nenda ilala boma asubuhi Kati ya saa 1 mpaka 5 utapata. Kama unaweza kusimama kwenye mnada kugombea Kwa kupandisha dau. Au unaweza kufika sehem moja maarufu hapo panaitwa "Ashanti". Ukifikishwa Ashanti Muulizie mtu anaitwa Muba au Ostadhi SELE. Hawa watu wawili wambie umepewa address na MJOMBA. Hao watakuuzia lakini elf 5 Kwa ubora wa ngu zao hawakuuzii. Ni bora uweke bei ya elf 8 (Standard) ambayo itakuruhusu uchague siku ANAYOFUNGUA.
NB. NI BORA UFIKE SIKU ANAYOFUNGUA BALO UPATE NGUO AMBAZO HAZIJACHAGULIWA SANA UKAUZE HARAKA KWA FAIDA NZURI.
Umejibu vizuri nitaenda na address yako ile hilo eneo la ashanti ndyo umeniacha mana mimi nataka za kuvaa tu.
 
Asee ninawaza kama nitaweza hii biashara. Mimi nimeajiriwa niweke mtu anisimamie. Kupata mzigo quality ndio changamoto ilipo nisije nikauziwa balo na malonya matupu.
 
Somo zuri sana bro. Mimi nina maswali machache.

1. Nikitaka kuanza biashara kwa kununua baro, la nguo, viatu na mabegi, nijipange na bei gani makadirio?

2. Nitaamini vipi kwamba ili baro ni quality? Niliambiwa yana bei tofauti tofauti.

3. Je, nitajuaje kama ilo baro limetoka nje (ulaya) isije kua kuna wahuni wanayafunga hapo hapo karume au Kariakoo wanatupiga sisi wageni ila quality wanauziana wanaojuana tu.

cc Sir Midabwada
Anhaa robota Mara nyingi zinagawanywa Kwa gredi. Kuna gredi A (1), B (2). Hizi zinatofautiana bei kwani gredi B huwa na nguo zlizochoka sana/Chanika kabisa NYINGI. hata bei huwa chini. Pia, hizi robota zinatofautiana nchi I. E Korea, China, Canada, Turkey. Mara nyingi ncchi hizi huathiri Sana Uonekanaji wa nguo (Fasheni, ukubwa au kuchoka).

Zinazotoka kanada Mara nyingi huwa saiz kubwa mnooo. Hapa tunawauzia vibonge /vipande Kam Msechu. Uturuki zinakosaga fasheni nzuri, ila waarabu wale wanapuliziaga udi sijui. Nguo zao hazitoi haruf y mtumba uliyoizoea (Karaha). Nguo za Korea na China ni nzur mno kwenye fasheni za kisasa. Nchi mbili hizi zinatoaga brand saw na tunazoziona madukani Kam starwar, Balenciaga n. K lakini pia Korea inajitahd kutoa nguo chache zlizochoka kufananisha na China.

SUALA LA UBORA WA NGUO NI RISKI. HUWA TUNATUMIA KUZIVUTA ZICHUNGULIE NJE THEN TUNAZIKAGUA MN'GAO. ZINAZOONYESHA KUN'GAA SANA TUNABEBA ROBOTA HILO. KWA KAWAIDA KILA ROBOTA HUWA LINAPEWA STICKER( NDANI YA NAILONI LAKE) KARIRI HIYO STIKA ITUMIE KAMA RIFAA, ZIKITOKA NGUO MBAYA HIZO STICKER ZIEPUKE UKIWA UNACHAGUA BARO. HII IMEKAA KIENYEJI ZAIDI
 
Asee ninawaza kama nitaweza hii biashara. Mimi nimeajiriwa niweke mtu anisimamie. Kupata mzigo quality ndio changamoto ilipo nisije nikauziwa balo na malonya matupu.
Kuweka mtu inawezekana ila jitahid awe muaminif na mzoefu Kwa mana awe na uwezo wa kunegotiate na watu tofauti (Rika, sifa, nk) na uchangamfu. Manake hii biashara hesabu ni mchezo wa kupatana. Nitakupa mikakati mmoja. Wewe pendekeza eneo unalotaka kubobea. Kwa mana Robota huwa zinafungwa kutegemea nguo Husika mfano. Jinzi Za kiume pekee, shati za mikono mifupi peke yake, bukta peke yake, jinzi za kike peke yake, suti peke yake, taulo na MASHUKA peke yake, za watoto peke yake, Kuna Robota hadi za Boksa za mtumba. Kwa Kujua lonya au Uzuri tumia mbinu hiyo hapo juu.
Lakini pia nahitaji Kujua unataka nguo za watu gani watoto, wanaume, wanwake, baibui au Nn unahitaji?
NB. Negotiation ni msingi mkuu wa faida ya biashara hii. Hawa jamaa wa mitumba hat ukiwaweka maduka ya unga wa sembe watanegotiate bei na wateja hata Kam bei inajulikan. Read article zinazowazungumzia machinga
 
Somo zuri sana bro. Mimi nina maswali machache.

1. Nikitaka kuanza biashara kwa kununua baro, la nguo, viatu na mabegi, nijipange na bei gani makadirio?

2. Nitaamini vipi kwamba ili baro ni quality? Niliambiwa yana bei tofauti tofauti.

3. Je, nitajuaje kama ilo baro limetoka nje (ulaya) isije kua kuna wahuni wanayafunga hapo hapo karume au Kariakoo wanatupiga sisi wageni ila quality wanauziana wanaojuana tu.

cc Sir Midabwada
Kuhusu mtaji mkuu kwa maeneo yote hayo unataka kununua Robota? Yan Robota la tisheti, ununue la mabegi, ununue la suruali alafu ufungue?.
Kama una mawazo ya Aina hii utapata hasara nzuri tu. Kila sehem hapo lazima uwe na CONSISTENT LEVEL. ili uweze kuendesha biashara hizo, mm binafsi bei ya Robota la viatu sijui. Kwa mana nikiingia anga za watu NAKULA ZA USO. ukitaka ufanye hii biashara Kwa amani hata m3. 5 inatosha vizur kabisa.

Pia,nikutoe katika wasiwasi hakuna mtu anaeweza kuandamiza nguo zile kwa Mkono au teknoloji ya kibongo kutoa Robota. Huwa Ina belt iliyokazwa mnooo. Robota ambayo haijachezewa au kuchomolewa nguo imeshikamana kama tofali
 
Kigezo cha nguo kuchoka Mara nyingi
1.uchakavu au matobomatobo
2.kwa jinzi huwa na zipu iliyoharibika au majinzi yasiyo na fasheni nzuri mf. Kuna suruali huwag chini Pana kuliko upana wa paja.
3. Kwa tisheti zisizo na Kola (ukosi) huwa zinatoaga dosari ya Kola PANA almaarufu 'MAMA NINYONYESHE'
 
Back
Top Bottom