Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,711
- 1,738
Ndugu yangu Nape wewe ni Katibu MUENEZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ufahamu wangu mdogo unatakiwa ukieneze chama chako kwa wananchi. Nilikuwa nakukubali katika mada mbalimbali zilizokuwa zikiandaliwa na vituo vyetu vya TV kwa kujikita katika MADA husika na ulijitahidi mno kutozungumzia UPINZANI hasa CHADEMA, lakini hivi karibuni sijui umepatwa na nini kwa kukusikia hata kwenye mikutano yenu ya CCM unakitaja CHADEMA.
Nadhani sasa unakolekea sio pazuri kwa faida ya chama chako na Taifa kwa ujumla, huna tofauti na Mwigulu Nchemba ambaye hata ukimkurupusha usingizini na kwa kumsabahi tu ataanza kutaja CHADEMA.
Kiumri bado una nafasi tu kukitumikia chama na Taifa letu hivo jikite katika kukitangaza chama zaidi kuliko CHADEMA kwani kufanya hivo ni sawa na kuwaingilia kazi yao.
Aksante mkuu, sahamani kama nakukwaza.
Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amen.