Naomba kujuzwa zaidi kuhusu chama kipya cha kutetea walimu (CHAKUHAWATA)

Yurri

Senior Member
Apr 29, 2015
176
227
Nina ufinyu wa uelewa juu ya chama hiki kipya cha walimu CHAKUHAWATA ( Chama cha kutetea Haki za Walimu Tanzania) ambapo ni chama mwenza cha CWT.

Natamani kujuzwa.
Mosi: katiba yao inapatikanaje?

Pili: Nafahamu ni chama kipya, sio rahisi Sana kuwa na ofisi kila wilaya kwa sasa, vipi kuhusu kimikoa, kikanda na hata kitaifa?

Tatu: wanatumia tovuti au wavuti ipi, (Media) njia ya kukijua chama husika

Nne: Nimepewa taarifa kuwa makato yao ni kwa amount, yaani Tsh.5,000/= na sio kwa % kama ilivo kwa CWT (Jambo hili linalowavutia Walimu wengi kujiunga na chama hiki kipya) Je, makato hayo yapo kikatiba au ni njia tu wakuvutia wateja (walimu) , baada ya kujiunga warudi kwenye mfumo wa kinyonyaji kama wa CWT wakukata kwa asilimia?

Tano: mwongozo wa namna ya kujiunga na chama hiki upoje?

Nawasilisha.

Asante!
 
Jitahidi uwajue Viongozi wa Chama kwanza kisha mengine yatafuata na utayapata kama ziada.
 
Jiunge kwanza na chama,hayo mengine utajifunza ukiwa ndani.
CWT wamekuwa hawana msaada kabisa na Waalimu,zaidi ya kufikiria matumbo yao.
 
Back
Top Bottom