Naomba kujuzwa vifaa vya ufundi Simu na Computer

Mtu anakuambia wiki tuuu watu wanarihisisha maisha aisee
Kuna fundi seremala alikua hana ishu mtaani akaomba kujifunza ufundi wa fastafasta wa kuokota buku 2 buku 3 haikuchukua zaidi ya mwezi amejua kutengeneza meza, stuli, frame za dukani, chaga za kitanda, kuchana mbao n.k.

We unataka jamaa aende chuo akajifunze kureplace system charge na kuflash simu mwaka mzima? Sio lazma ulivostruggle wewe shule na mwenzako astruggle hivyohivyo, mfanyie wepesi apate hela ya kula, hayo makuu atakuja tu kuyajua taratibu.

Kariakoo tunaona vijana wanyoa viduku wana vibanda vyao vidogo wanafanya ufundi, wale unataka kusema wameenda chuo?
 
haujui ufundi mimi nipo kwenye huo ufundi kwa muda mrefu kuna vingi vyakujifunza sana wewe uelewa wako umeishia kwenye system Charge halafu ukimpa simu akikuulia uje ulalamike huku
Hawezi kuua akiwa chini ya uangalizi wako, unakua supuervisor wake, akimaliza kutengeneza unahakiki
 
Nimekutana na mafundi wengi wa simu mtaani wanasema wanabadilisha System charge.

Hii ni moja kati ya matatizo ya uelewa kwa mafundi ambao hawana elimu ya Electronics au computer.

Kwa mfano: "System charge" kwanza sio Neno sahihi ,
Neno sahihi ni "Charging System" au " Charging Pcb".

Kile wanachokiita System charge sio sahihi , bali ni "Power Connector" au "USB Jack" au "USB Connector"

Sasa kwa fundi aliyepitia mafunzo aidha ya ufundi simu au Electronics, kwake inakuwa rahisi kwanza kujua anafanya nini? Na pia kumuelewesha mteja nini kinahitajika.

Elimu rasmi ni muhimu kwa ufundi bora.
 
Vifaa vya ufundi simu

1😱pening toolS
2:soldering tools
Hot gun
Soldering gun
Flusk

3:Test and repair tools
Multimeter
Test cable

4:dc power supply

5:software tool
Computer
Dongle
Flash box

6.pcb Holder

7:BGb tool

8:cleaning tool

9:water damaged tool
Ultrasonic cleaner

10:light tool

11:lcd refurbished tool

12😛hone repair hand tool
Tweezers
Repair mat
13:soldering microscope

Na vingine vingi jitahidi kupata vifaa bora lakini unaweza kupata Kariakoo vifaa vya kiwango kidogo ila ukiwa seriously na kazi vifaa garama yake ni kati ya m4 kariakoo vifaa vyote ni kama 1m ila baadhi ya vifaa ubora ni duni
 
Asante sana mkuu
 
Chief huyu inabidi ajifunze ule ufundi njaa yani anajua tu zile basics ili apate hela huku vitu vingine akiwa anaendelea kujifunza kidogokidogo. Mchukue hata wewe umpige msasa mbona kazi ni zilezile hamna jipya?
Asifanye ufundi njaa ni bora atafute fundi mbobezi awe chini yake aweze kujifunza au kuelekezwa hadi pale atakapopata mwanga wa kazi hiyo.

Mwaka mmoja hauwezi ukawa umejifunza mambo yote yanayohusiana na ufundi wa simu ukawa umemaliza. Karibia kila jamii ya simu ina muundo wake wa utatuzi wa matatizo, kuanzia ufunguaji, ubadilishaji wa kifaa kibovu, na ufungaji pasipo kudhuru kifaa kingine.

Kuna uundaji wa kifaa mbadala kama kile cha mwanzo kimekosekana (mfano; mic za njia 4 au zaidi, mwanga wa kioo au charging ic).

Ufundi wa simu ni fani inayohitaji uelewa na umakini wa hali juu, kuna uharibifu huwa unatokea hata kama ni mzoefu, mfano, kukata finger print, kuvunja kioo au tachi, kuvunja au kuunguza connectors na kutoboa betrii. Matatizo haya huwa yanawakumba mafundi na fundi anaweza akatatua tatizo alilolisababisha kwa kumshirikisha mteja au anapambana nalo akalimaliza.

Upande wa Software ndipo simu nyingi zinapokufa sana kuliko upande wa hardware, Kuna kuflash simu kwa file ambalo sio sahihi, au file ni version ndogo, au emmc imefikia kikomo cha matumizi simu ikazimika pia kuna kufuta partition zinazohusika na network. Hapa ndipo inahitajika elimu zaidi ya namna ya kubadilisha emmc, power ic na cpu na kwenye mafundi zaidi ya 50 unaweza ukakuta mafundi 4 tu ndio wenye uwezo wa kucheza na hizo sehemu 3 emmc, power ic na cpu.

Kwenye Software hautakiwi ujuwe kutumia programu ya kuflash kwa kuload file na kuflash tu, bali inabidi ujue mfumo wa utendaji kazi wa simu kwa kila partition iliyopo kwenye simu kabla haujasababisha hasara. Inatakiwa ujue kile unachokifanya baada ya zoezi nini kinatokea.

Kama ni ufundi njaa ajifunze kuchoma mic, vioo, speaker, ringer na jamii ya vitu kama hivyo.

Hata hapo kariakoo hao wanaojiita mafundi sio wote, wengi ni madalali wa ufundi, anapokea kazi anampelekea fundi mwingine anayeweza zaidi yake.
 
N kweli asee
 
Back
Top Bottom