Hizi hapa ni shule ambazo ninazifahamu ambazo zinafanya vizuri Kitaaluma na maadili na ada zao zina nafuu kiasi fulani.
1. Centennial Christian Seminary- Iko Kongowe ya Kuelekea Mkuranga. Ni ya mchanganyiko na inaendeshwa na Wamisionari kutoka Korea. Mtoto awe vizuri kichwani, bila hivyo hachukuliwi. Tovuti yao hii
Centennial Christian Seminary - About CCS
2. Mwandege Boys- Hii iko kijiji cha Mwandege wilaya ya Mkuranga- mbele kidogo ya Kongowe na ni kwa ajili ya wavulana
tu.
3. Stanley Sec. School. Iko Toangoma Kigamboni na ni mchanganyiko
4. Mwenyeheri Anwarite- Ipo Ubungo Kibangu- ni mchanganyiko.
Unaweza pia kutembelea tovuti ya Baraza la Mitihani (NECTA) ili kuangalia matokeo yao ya mitihani kwa miaka ya karibuni.
Natumai nitakuwa nimekusaidia kwa kiasi kwa kadiri ya ufahamu wangu kuhusu hizo shule.