Naomba kujuzwa dawa ya kutibu tatizo la kichwa kuuma mara kwa mara

Manstone

JF-Expert Member
May 12, 2013
511
310
Habari wapendwa?

Nakuja kwenu kuomba anaefahamu dawa ya maumivu ya kichwa kwani yamekuwa yananisumbua kila siku najikuta natumia painkiller kila aina lakini zinagonga mwamba huu mwaka was saba sasa kinanisumbua tu.

Nimeenda hospitali mbalimbali lakini naambiwa sina, nimepiga CT scan MRI sins tatizo lolote. Blood pressure,damu na macho vyote viko sawa.

Nikaambiwa tatizo ni kichwa cha migraines nimetumia dawa we kinapoa mda wa masaa 2 mpk 3 kinaanza tena imefika mpaka hatua sasa nakunywa dawa kichwa maumivu hayaishi kabisa.

Naombeni wmenye mawazo, dawa au ushauri anipe jamani nimechoka.
 
1: Unahitaji kusikilizwa na kufanyiwa tathmini upya kama kweli tatizo ni migraine.

2: Kama ni migraine, huwa kuna dawa za kutibu na kuzuia.

3: Kama ni migraine, zaidi ya dawa kuna haja ya kuwa na mabadiliko ya kimaisha kwa ujumla ili kupunguza baadhi ya vitu vinavyoanzisha attack kama:

A: Mwanga mkali

B: Harufu kali/ pafyumu

C: Matumizi ya pombe

D: Stress

E: Matumizi ya mtindi, kahawa na chocolates

D: Vyakula vya kusindikwa/makopo na soda

F: Usikae na njaa muda mrefu

G: Kutokuvuruga ratiba yako ya usingizi na uwe wa kutosha (saa 8).

H: Kwa akina mama, asitumie mfumo wa homoni wa uzazi wa mpango.

I: Usiwe mtu wa kukasirika mara kwa mara.

J: Kutokujichosha sana/kupita kiasi.

K: Kunywa maji ya kutosha, kulingana na eneo ulilopo, uzito wa mwili na aina ya kazi.

L: kujiepusha na maeneo yenye sauti kali/kelele.
 
We jamaa utakua Dr. Unaongea vitu vina reflect kwangu
 
Kwanza msihi Mwenyezi Mungu akuponye, akuongoze kwa kupata matibabu sahihi.

Kama una hela nenda ng’ambo ukafanya uchunguzi zaidi na kupata kupona.
 
Kuna kurogwa pia.

Nenda kwa Mmwamposa ukakutane na nguvu ya Mungu kwa rehema zake utapona itabaki historia,

Actually sio kwa mwamposa tu Hata kwenye huduma nyingine watu wengi wana pokea miujiza ya uponyaji .
 
Matapeli wote hao

Kumbuka anayeponya ni Mwenyezi Mungu.

Hao jamaa pamoja na madhaifu yao lakini Mungu anaweza kuwatumia kama vyombo ktk kuwaponya watu.

Mwenyezi Mungu anaweza mtumia mtu yeyote kwenye kazi yake bila kujali holiness status ya mtu huyo.

Ijapokuwa kusema ukweli Mwenyezi Mungu anapendezwa na mtu wa haki na utaua.
 
Back
Top Bottom