Naomba kujuzwa chanzo cha tatizo la kipanda uso na suluhisho lake

Knju

Member
Aug 26, 2017
31
125
Wakuu poleni na majukumu ya kikazi. Naombeni msaada wakuu wangu hivi tatizo la kipanda uso linasababishwa na nini? Na je kuna tiba ya kuliondosha tatizo hilo?

Mwenye kujua naombeni msaada wakuu wangu.
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,442
2,000
Wakuu poleni na majukumu ya kikazi. Naombeni msaada wakuu wangu hivi tatizo la kipanda uso linasababishwa na nini? Na je kuna tiba ya kuliondosha tatizo hilo?

Mwenye kujua naombeni msaada wakuu wangu.

1599597479110.png

Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni ashirio la matatizo ya kiafya ambayo yame-advance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.

Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo:

- Mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
- Baadhi ya neva za fahamu zilizoko usoni

Misuli ya kichwani
Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazina mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.

1: Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.

2: Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.

3: Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.

4: Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.

5: Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.

6: Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.

7: Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.

8: Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .

9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10: Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.

11: Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.

12: Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.

Kabla ya kukupa dawa na ushauri wangu nina maswali nikuulize unijibu.

Je unapata Usingizi wa kutosha? Unalala usiku masaa mangapi? Je, unakunywa maji ya kutosha? Una miaka mingapi? Unapata haja kubwa ya kutosha? Nenda pia kapime macho yako na ukapime tena kwenye mishipa yako ya fahamu huenda una matatizo. Na kitu kingine unakuwa upo juani uwe unavaa kichwani kofia.

DALILI ZA KIPANDA USO
Kipanda uso (Migraine) ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa anayokuwa nayo mtu baada ya mshipa wa damu (Enlargement of Artery ) kutanuka katika kichwa chake.

Baada ya kutanuka kwa mishipa hii ya damu, pia kuna kemikali ndani ya mwili zinazozalishwa na kuizunguka mishipa hii na kupelekea mtu apate maumivu makali ya kichwa na kutanuka zaidi kwa mishipa.

Maumivu makali ya kichwa hupelekea mfumo wa utendaji kazi wa mwili pia ubadilike, mtu atapatwa na kichefuchefu, kutapika, kuharisha, katika utumbo chakula hakitanyonywa vizuri kiingie mwilini, mtu atashindwa kuona vizuri maeneo yenye mwanga na kutopenda kukaa mazingira yenye sauti au kelele.

Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuchangia mtu apate tatizo la kipanda uso, vitu hivi haimaanishi kuwa ni lazima kusababishe upate na hata kama haupo katika mazingira ya vitu hivi haimaanishi kuwa huwezi kupata tatizo la kipanda uso, miongoni mwa vitu hivyo ni kama vile: sauti kali au kelele, harufu kali, aleji, mwanga mkali, kuvuta sigara, matatizo ya kukosa usingizi, kukaa bila kula kwa muda mrefu, pombe, kubadilika badilika kwa siku za mwanamke (menstrual cycle fluctuations).

Inawezekana ukawa na tatizo hili la kipanda uso, miongoni mwa vitu vinavyowasaidia watu wenye kipanda uso ni kutumia dawa mbalimbali ukijumuisha dawa za maumivu zenye mchanganyiko na caffeine, pia utumiaji wa chai au kahawa umesaidia baadhi ya watu kuwapa nafuu ya maumivu makali ya kichwa.

Tunaweza kupunguza hatari (risk) ya kupata kipanda uso kwa kubadilisha staili ya maisha yetu ya kila siku, kuepuka vitu vyenye harufu kali, kuepuka utumiaji wa tumbaku (sigara), kupata muda wa kutosha kuupumzisha mwili (kulala), kufanya mazoezi, kutokaa bila kula kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha.Je, unalo tatizo la kipanda uso (Migraine), dalili zako ni zipi na ni vitu gani ukitumia unapata nafuu?
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,442
2,000

AINA KUMI NA MBILI ZA KUUMWA NA KICHWA

Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni hashirio la matatizo ya kiafya ambayo yameadvance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.

Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo.mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
Baadhi ya neva za fahamu zizlizoko usoni
Misuli ya kichwani

Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishuu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazna mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.

1: Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.

2: Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.

3: Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.

4: Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.

5: Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.

6: Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.

7: Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.

8: Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .

9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10: Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.

11: Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.

12: Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.

Ushauri wangu nenda hospitali kapime damu unayo damu ya kutosha? Nenda kapime macho? Je unapata Usingizi wa kutosha? Je unatapa choo laini kwa wiki unakwenda haja kubw amara ngapi? Je uanyo mawazo au Stress? Kapime Mapigo ya Moyo wako (High blood Pressure ) Yanakwenda sawa? Kisha uje hapa unipe majibu
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,442
2,000
KIPANDA USO (MIGRAINE) NI DALILI YA UGONJWA WA KIHARUSI

Kwa ufupi

Zipo sababu za ugonjwa huu. Wagonjwa tofauti wanaweza kuhisi moja ya kati ya nyingi zilizopo. Unaweza kutokana na kufinywa au kupungua kwa upenyo wa mishipa ya damu inayopeleka damu sehemu ya mbele ya ukuta wa jicho au au mabadiliko kwenye mshipa wa fahamu wa jicho (optic nerve).

By Dk Isaack Maro

Kipanda uso cha macho ni maradhi yanayosababisha maumivu ya kichwa yakiambatana na matatizo ya macho. Maumivu haya huweza kutokea bila dalili zilizozoeleka za kipanda uso na mara nyingi husababisha kuona kwa shida au kutoona kabisa kwa kipindi kinachozidi saa moja.

Zipo sababu za ugonjwa huu. Wagonjwa tofauti wanaweza kuhisi moja ya kati ya nyingi zilizopo. Unaweza kutokana na kufinywa au kupungua kwa upenyo wa mishipa ya damu inayopeleka damu sehemu ya mbele ya ukuta wa jicho au au mabadiliko kwenye mshipa wa fahamu wa jicho (optic nerve).

Yaweza pia kutokana na maradhi yanayohusisha mfumo wa damu kama vile seli mundu au mwanga mkali unaomulika ghafla machoni. Pengine ikawa harufu kali ya marashi au sauti kubwa.

Msongo wa mawazo, wasiwasi na unywaji wa pombe kupita kiasi ni sababu nyingine. Hata unywaji wa kiasi kikubwa cha kahawa nayo husababisha bila kusahau mabadiliko ya hali ya hewa.

Ugonjwa huu unaweza kumpata yeyote lakini wenye historia ya kuugua wapo kwenye hatari zaidi. Tafiti za kisayansi zinaonyesha maradhi haya hurithiwa. Hii ina maana familia ambazo zina historia ya watu waliowahi kupata maradhi haya huwa kwenye hatari zaidi.

Kipanda uso cha macho kina uhusiano na homoni ya kike inaiitwayo Oestrogen hivyo kumaanisha huonekana zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Siyo tu huonekana zaidi kwa wanawake bali kwenye vipindi fulani kutokana na kuongezeka au kupungua kwa homoni hizo, mfano kipindi cha hedhi.

Kipanda uso cha macho huwa na dalili zinazofanana na kipandauso cha kawaida kama vile kichwa kuuma, kupata kizunguzungu, kusikia kichefu chefu na mara nyingine kutapika.

Ingawa dalili nilizotaja hapo juu huwa zinaonekana kabla au wakati wa maumivu makali ya kipanda uso si mara zote hutokea kwenye kipanda uso cha macho.

Kuumwa kichwa unapotazama mwanga mkali au kusikia sauti ya juu ni dalili nyingine ya ugonjwa huu. Lakini dalili kubwa ya kipanda uso cha macho ni kuona taswira ya vitu kama nyota au mwanga mkali wa mistari mistari.

Wengine huona giza muda mfupi kabla tatizo kutokea. Dalili ya kuona mwanga mkali wenye nyota nyingi ni dalili inayoripotiwa na wagonjwa wengi zaidi. Hali hii hudumu kwa kipindi kifupi kisichozidi dakika sitini au saa moja.

Tafiti zinabainisha dalili za maradhi haya mara nyingi hufanana na za maradhi mengine hivyo mgonjwa anatakuwa amuone daktari ili vipimo vitakavyothibitisha.

Historia ya maradhi na vipimo vikionyesha kuwa kweli tatizo la mgonjwa ni kipanda uso cha macho basi atapewa dawa za kutuliza maumivu ya kichwa na kuzuia kuongezeka kwa shinikizo la damu kwenye macho.

Yapo madhara ya kipanda uso cha macho ambacho mara nyingi husababisha maumivu makali ynayaomfanya mgonjwa kushindwa kufanya shughuli zake za kawaida ingawa huwa haudumu kwa muda mrefu.

Mara nyingi kipanda uso cha macho huwa ni ishara ya maradhi mengine makubwa na yenye matokeo mabaya zaidi. Ugonjwa huu unaweza kuambatana na majeraha au uvimbe kwenye ubongo.

Pengine waweza kuwa dalili ya kiharusi au kutanuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo (aneurysm) kama siyo maradhi ya mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye ubongo.

Yaweza kuwa ishara ya maumivu ya mishipa ya fahamu au kichwa kikubwa (hydrocephalus) hasa kwa watoto. Wakati mwingine humaanisha upungufu katika maumbile ya fuvu la kichwa.

Chanzo: Kipanda uso ni dalili ya ugonjwa wa kiharusi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom