Naomba KUJUA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba KUJUA

Discussion in 'JF Doctor' started by nsyagile, Nov 14, 2011.

 1. nsyagile

  nsyagile Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nini tiba ya miguu kuvimba kuanzia kwenye vifundo(joint) hadi vidoleni
   
 2. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,355
  Likes Received: 2,361
  Trophy Points: 280
  Kwani una mimba?Nijibu ili nikuelezee.
   
 3. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,355
  Likes Received: 2,361
  Trophy Points: 280
  Kwani una mimba?Nijibu ili nikuelezee.Nisamehe kama we ME na sio KE.
   
 4. nsyagile

  nsyagile Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpendwa wangu sina mimba na tatizo hili limenianza tangu 2002 nimetembea hospitalim nyingi napimwa lakini bado sijapata tiba sahihi. zamani ilikuwa inavimba nakupungua baadaya ya wiki nilikuwa naweza kukaaa miezi kadhaa lakini sasa tatizo limekuwa kubwa ndani ya mwezi inweza kupungua siku mbili mpaka tatu siku ziliozobaki inajaa na ninajisikia kizunguzungu muda wote.
  Tafadhali nisaidie kama unajjua tiba
   
 5. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pole sana ndugu kwa tatizo linalokusumbua, huo ugonjwa kwa kitaalamu unaitwa pedal edema. Na yenyewe huweza kuwa ni dalili za ugonjwa ambao uko ndani ya mwili wako. Kwa kina dada wanaovaa viatu vinavyo kaza sehemu ya vifundo vya miguu, husumbuliwa sana na tatizo hili na wao hupona wanapoacha kuvaa viatu vya aina hiii. Pia ugonjwa huu unaweza kutokana na watu wenye tabia ya kula chumvi kwa kiasi kikubwa na hasa ile chumvi ya kuongezea mezani. Lakini pia ni vizuri ukaenda kwa wataalamu wauchunguze mfumo wako wote wa damu (cardiovascular) system, na mafigo pamoja na ini vyote hivi husababisha matatizo haya.
  Lakini kama tiba jitahidi kuepuka kukaa kwa muda mrefu, au hata kama umekaa nivizuri kunyoosha miguu juu ya kitu kingine ili paja na kikanyagio (foot) viwe kwenye level moja usining'inize miguu kwa muda mrefu. Epuka utumiaji wa chumvi uliopindukia, Fanya mzoezi ya viungo mara kwa mara na punguza uzito.
   
 6. nsyagile

  nsyagile Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana nitajitahidi nifanye kama ulivyonishauri japo nimeenda hospital nyingi ikiwa ni pamoja na muhimbili, regency n.k labda sijabahatika kukutana na mtaalam aliyebobea.
   
Loading...