Naomba kujua tofauti ya haya maneno

jitupori

Senior Member
Feb 22, 2015
199
76
Watu wengi nimewasikia wakitamka neno 'embu' na kwa upande mwingine nimewasikia wakisema 'ebu' na wengine pia 'hebu' mfano;
Mtu wa 1:embu niletee maji
Mtu wa 2:ebu niletee maji
Mtu wa 3:hebu niletee maji

Hivi nani atakuwa yupo sahihi kati ya hao wa 3???
 
Yote yana maana sawa isipokuwa yanaandikwa na kutamkwa tofauti kulingana na kanda ya mtamkaji kwa mfano Pwani: emb(u), Kanda ya Ziwa : hebu/ebu
 
Yote yana maana sawa isipokuwa yanaandikwa na kutamkwa tofauti kulingana na kanda ya mtamkaji kwa mfano Pwani: emb(u), Kanda ya Ziwa : hebu/ebu
Naomba kupingana na wewe , waswahili wengi hutumia " HEBU " ambalo Kwa wale H inowapa matatizo husema " EBU" na wengine ni hilo " EBU " ila sifikirii kama ni neno sahihi.
 
Naomba kupingana na wewe , waswahili wengi hutumia " HEBU " ambalo Kwa wale H inowapa matatizo husema " EBU" na wengine ni hilo " EBU " ila sifikirii kama ni neno sahihi.
Ndo maana nikasema anaetamka "emb" au " ebu" huwa na maana ile ile sawa na aliyetamka "hebu" kulingana na mazingira au ukanda anakokaa.
Hii lugha kuna watu wqmameiharibu sana kutokana na lugha zao mama.
 
Back
Top Bottom