Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 251
- 638
Habari za muda huu wana JF
Mwenye elimu kuhusu haya mswala au mwenye uzoefu wowote Naomba kujua maana ya hii ndoto. Nitaandika vile ninavyovikumbuka, vinaweza visiwe na mtiririko mzuri lakini nitajitidi muweze kuielewa
Niliota nimepewa taarifa ya msiba wa mtu ambae niwa karibu yangu sana, mtu niliempenda sana, (mzazi wangu) . Cha ajabu sikustuka wala kulia. Tukiwa njiani kuelekea msibana mahali ambapo watazika nikakumbuka kuwa niliyeambiwa amefariki alishafariki miaka mingi iliyopita
Nikapata mstuko, nikamuuliza mtu aliyekaribu yangu "samahani mbona huyu tunaeenda kumzika leo alishafiriki miaka mingi, imekuaje?" akanijibu "hapana aliyefariki ni mwingine ila majina yanafanana tu"
Baada ya kujibiwa hivyo ghafla mwili wa marehemu ukawa umewasili wakaenda kuupokea na kufanya maandalizi ya kuaga pamoja na kuzika. Cha ajabu aliyefariki hakuwa mmoja kama nilivyodhani bali walikuwa watu wawili.
Muda wa kuaga ulipofika mimi nilikataa kwenda kuaga, nililazimishwa sana tena sana ila nikajikuta nakataa huku nikadai eti aliyefariki sikuwa namjua wala simfahamu ya nini nimuage. Watu walinishangaa na kuniacha
Nilipojaribu kuwaangalia kwa mbali wale waliofariki ambao watu wanasema wamefanana majina na yule niliedhani kafa muda mrefu, nilistuka sana kwa jinsi nilivyowakuta.
Kwanza majeneza yao yalikuwa tofauti na majeneza ya watu wengine, yalikuwa yanawaonesha mwili mzima. Alafu sasa mmoja kati ya wale marehemu wawili alikuwa amelala chali lakini mikono kaichanua huku na huko. Marehemu wa pili alilala kawaida kama marehemu wengine wanavyolazwa.
Cha ajabu yule alielala kawaida akaamka, lakini watu hawakustuka wala kukimbia ni kama hawakuona chochote. Mimi nilistuka sana, mpaka yule marehemu akaniona. Akaniuliza "wewe unaniona.?" nikamjibu ndio kwa kutikisa kichwa
Alikasirika sana, akakunja sura akaniuliza tena nikamjibi hivyo hivyo. Safari ya tatu akawa anamtikisa marehemu mwenzake na kumwambia "huyu anatuona, amka kuna mtu anatuona....." akawa anamwambia huku ananisogelea na sura kaikunja kwa hasira.
Nilipata hofu ya ajabu na ghafla nikastuka usingizini, nilikuwa nahema kwa nguvu moyo unadunda na natokwa jasho jingi.
Kiukweli hii ndoto nimeota muda kidogo kama miezi miwili hivi lakini mpaka leo inanitesa. Kila nikikaa mwenyewe naikumbuka. Nimeota ndoto nyingi za kutisha tena zaidi ya hii lakini hii nashangaa haitoki kichwani mwangu.
Naomba mwenye kujua maana yake, au anaemjua mtu anaeweza niambia maana yake amTag. Nahitaji kujua. ASANTENI