Naomba kujua, ndege ya Rais iko wapi?

Naomba kujua, ndege ya Rais iko wapi?

Nitajulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2017
Posts
328
Reaction score
355
Wapendwa habari za majukumu,

Naamini kila mtu atakuwa anajua kuwa serikali ya awamu ya NNE ilinunua ndege kwa ajili ya safari za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania almaarufu "Ndege ya Rais"

Sasa tokea serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani sijaona Rais akisafiri nayo safari na hasa zile za mbali. Naomba kujua hiyo ndege iko wapi na inafanya kazi gani?!!!
 
Labda ATCL wamepewa kuziba pengo la bomba waliogomea weupe kuileta
 
Kwani sasa anatumia ndege gani mikoani,kama sio hiyohiyo?
 
Utaambiwa imepelekwa jeshini... ili usihoji tena.. ngoja wajuvi waje watakupa majibu safi kabisa.
 
IPO nadhani ila Raiis anapendelea usafiri wa barabara lakini so vibaya wahusika wakamjibu.Kisa-wiki iliyopita jijini Mwanza kulikuwa na mvua.Ndege zingine za abiria zilishindwa kutua na kwenda kutua Kilimanjaro lakini bombardier ya ATC ilitua ikanyanyuka ikaenda Bukoba ikarudi ikatua tena na ikanyanyuka ikapaa tena kwenda Dar kwenye mvua hizo!
 
Hiyo ndiyo tulijibana kwa kula mboga mboga ili inunuliwe Gulf stream 550 aka 5H_one. Tukiachana na ile Dutch fokker 28 ambayo maraisi wametumia kwa muda mrefu. Wanaojua zaidi watakuja mimi nimeanzisha utangulizi tu.
 
kwani uwanja wake wa chato umekamilika
 
kwani uwanja wake wa chato umekamilika
536a71b7934bf9036e0a2367ca3bb78a.jpg


Chattle Airport. Iko tayari mkuu
 
Wapendwa habari za majukumu,
Naamini kila mtu atakuwa anajua kuwa serikali ya awamu ya NNE ilinunua ndege kwa ajili ya safari za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania almaarufu "Ndege ya Rais"
Sasa tokea serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani sijaona Rais akisafiri nayo safari na hasa zile za mbali.Sasa naomba kujua hiyo ndege iko wapi na inafanya kazi gani?!!!
Ndege ipo. Na mheshimiwa anaitumia.
Na ndege hiyo ilinunuliwa wakati wa awamu ya tatu si awamu ya nne
 
apart from usumbufu wa barabarani kwa wananchi kutokana na misafara mirefuuu ivi cost ya kutumia ndege na misafara ipi ni cheap
 
Back
Top Bottom