Naomba kujua kuhusu biashara/soko la viazi vitamu

Bolingo Ya Telephone

Senior Member
Jun 29, 2020
114
116
Wakuu, naomba kujua machache kwa wenye uzoefu na masoko ya viazi vitamu. Nina shamba langu la viazi vitamu,nitaanza kuvuna mwezi wa nane,nategemea kuvuna zaidi ya gunia 200.

Sasa naomba kujua hali ya masoko hasa kwa walioko Dar es Salaam,vipi bei ya gunia la kilo 100 linauzwaje huko? Au wanauza kwa kilo? Naomba tushirikianeni ili tupate taarifa ya kutosha kuhusu masoko ya zao hili.Ahsante!
 
Kwema mkuu. Nikipita hapa gongo la mboto wanapima kwenye ndoo kwa kina mama wanaokwenda kukaanga. Au unapewa vya hela uliyonayo wanakuhesabia. Ili upate faida nzuri vuna leta hapa unaweza kuuza jumla au rejareja wewe tuu mkuu.
 
Ahsante sana mkuu,pamoja sana
 
Viazi vitamu Tumelima wengi sana mwaka huu! Mie nimeamua kula mwenyewee tuu...Nikiangalia hiyo bei bora nile tu.
 
Bei kwani ikoje mkuu. Hebu lete niione. Maana viazi kila wiki nanunua na kipimo na bei ni ile ile iko costant. Wewe uko wapi mkuu?
 
Mahalia ambapo niliwahi kuona bei ina fluctuate ni shinyanga. Ambapo wanavikata vidogo vidogo wanakausha na wenyeji wa kule ndio kitu wanapenda sana.

Ikiwa ni viazi lishe ndio soko zuri zaidi maana inatengeneza vitu vingi sana. Unga wa uji, jwisi, unga wa mikate na vitu vingine vingi.
 
Mkuu nenda soko la Mabibo Dar muulize dalali wa viazi vitamu anaitwa Roger, biashara wanafanyia kwenye mwembe karibu na NIT.
Atakupa muongozo bei ya gunia moja kiasi gani, ulinzi, kupakia na kushusha mzigo, n.k.

Bei hubadilika kutokana na mahitaji ya wakati huo.
Bei zinaanzi 60,000/= hadi 80,000/= kwa gunia 1.

Hao watakupa na muongozo wa usafiri n.k.
 
We ndie umeongea kwa biashara ya viazi ukiwa jijini ama mkoani wasiliana na watu wa soko la mabibo tu, hao ndo wataalamu. Wakikuamini watakupa taarifa nyingi Sana ambazo ni fAida kubwa kwa mnunuzi na muuzaji.
 
Mkuu nenda soko la Mabibo Dar muulize dalali wa viazi vitamu anaitwa Roger, biashara wanafanyia kwenye mwembe karibu na NIT.
Atakupa muongozo bei ya gunia moja kiasi gani, ulinzi, kupakia na kushusha mzigo, n.k.

Bei hubadilika kutokana na mahitaji ya wakati huo.
Bei zinaanzi 60,000/= hadi 80,000/= kwa gunia 1.

Hao watakupa na muongozo wa usafiri n.k.

Dah! Mkuu nashukuru sana kwa haya maelezo.
 
Ekari moja huwa inaweza toa gunia ngapi ikitunzwa vizuri? Tuchukulie mita 70 kwa 70 tunazoziita ekari moja mtaani.
 
Vikikudodea lisha mifugo, hamna hasara hapo.Viazi,mihogo vinatakiwa vikutane na ramadhani ndio utauza being nzuri, vinginevyo ubahatishe.
 
Kama ww ni mkulima na huna dalali mabibo utapata tabu sana kuuza mazao yako dar labda uwe na tenda kwa watu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom